0657128567

Mwanza Tanzania,

Karibu Sana Kwenye Mtandao huu Wa Shule Tanzania

Showing posts with label MAFANIKIO. Show all posts
Showing posts with label MAFANIKIO. Show all posts

Sunday, April 22, 2018

ANZIA HAPO ULIPO

Muda sahihi wa kufanya maamuzi ilikuwa miaka 10 iliyopita, lakini muda mwingine sahihi wa wewe kuchukua hatua ni leo, huhitaji kuwa sahihi ili uweze kuanza, anza tu, Mungu atabariki!!

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

Pius J. Muliriye
Whatsapp|0717375782

Thursday, February 22, 2018

MAMBO NANE (8) MUHIMU SANA YA KUFAHAMU KABLA YA KUTENGENEZA BATIKI.

Habari rafiki yangu, naamini unaendelea vizuri na mapambano ya kuboresha maisha yako.

Kama ilivyo kawaida yangu nakufunulia fursa mbalimbali ambazo ukiamua kuchukua hatua unaweza kubadili maisha yako kabisa. Cha msingi sana ni kuchukua hatua.

Leo nakuletea fursa ya kutengeneza batiki, fursa ambayo si wengi sana wanaijua kwa maana ya jinsi ya kutengeneza, hata kama watu wanajua kutengeneza bado hawachukui hatua na kufanya fursa hii kuwa ya wachache na imewatajirisha wengi sana na wengine maisha yao yamebadilika kabisa.

Nisikuchoshe sana ndugu, leo hii nakuletea list ya vitu muhimu au mambo manane (8) ya muhimu kuyajua kabla ya kuanza kutengeneza batiki yenye ubora wa hali ya juu. Vitu hivyo ni:-

MAHITAJI:
1.Vibao vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa
7. Jiko.

MADAWA:
8.Sodium hydrosulphate.
9.Caustic soda
10.Mshumaa.

KAZI ZAKE:
1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.
2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

Zifuatazo ni picha za baadhi ya batiki ambazo ninatengeneza na kuwauzia wateja wangu.

















Je unatamani kujua kutengeneza batiki?? Hii ni miongoni mwa fursa zilizojificha kabisa na watu hawazioni na hata kama wanaziona hawachukui hatua yoyote, kama unasoma makala hii na unasikia moyoni unatamani kujua jinsi ya kutengeneza batiki hizi basi naamini ndani ya muda mfupi unaenda kuwa mtu mwingine kabisa.

Inawezekana kabisa unajiuliza kuhusu mtaji inagharimu kiasi gani, nataka nikutoe hofu, mtaji wake ni kiasi kidogo saaaana ambacho huwezi kuamini, na utajiuliza kwa nini watu hawafanyi biashara hii kwa wingi na wakati mtaji ni kiasi kidoooooogo sana, nimeshasema sababu hapo juu ni kwamba watanzania wengi hatupendi kujishughulisha, tunapenda kukaa vijiweni kulalamika maisha magumu tu na kuzungumzia maisha ya watu. Ninaamini baada ya kusoma makala hii utakwenda kuchukua hatua mara moja.

Nina habari njema kwa wewe ambaye umependa kujifunza mradi huu.

Kama uko serious na unataka kujifunza jinsi ya kutengemeza batiki basi nimekuandalia kozi maalumu kwa ajili yako.
Kozi hiyo itakufundisha kwa kina, hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza batiki yenye mikunjo/michoro mbalimbali ya kupendeza machoni pa watu.

Kozi hiyo itakuwa kwa njia ya VIDEO ambayo itakusaidia kuangalia kwa vitendo jinsi tunavyokunja mikunjo hiyo na kuweka rangi mbalimbali.

Je uko tayari???

Kama uko tayari niandikie ujumbe whatsapp 0717375782 kwamba uko tayari kujifunza BATIKI kwa njia hiyo kisha nitakuingiza darasani. KARIBU SANA.

Najua bado unajiuliza mtaji ni shilingi ngapi???? Najua vijana wengi tukitaka kuanza mradi flani tunawaza sana kuhusu mitaji. Nataka nikwambie kwa mradi huu hata sh. 15,000/- unaweza kutengeneza batiki nzuri na watu wakabaki kukushangaa. Pia utakuwa unajiuliza nitatoa wapi malighafi???? nataka nikutoe hofu, Tanzania sasa ni ndogo sana, kama hutapata sehemu au mkoa uliopo tutakutumia popote ulipo ilimradi tu utimize ndoto zako. Usiogope, chukua hatua sasa, natamani sana kukuona darasani.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

Pius J. Muliriye
0717375782 | whatsapp tu.
0754745798 | meseji tu (usipige)
piusjustus28@gmail.com
www.piusjustus.com

Tuesday, February 13, 2018

JINSI YA KUWA MJASIRIAMALI WA MTANDAO.


Sunday, February 11, 2018

Njia 14 Halali za Kupata Pesa Kupitia Blog

Je unatafuta njia ya kujipatia pesa kwenye mtandao ambayo siyo ya utapeli? Blog ni njia moja wapo unayoweza kuitumia kujipatia fedha huku ukifanya kile ukipendacho. Katika makala hii nitakushirikisha njia 14 unazoweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia blog yako.



Kumbuka! Hizi si njia za kupata pesa za mteremko haraka haraka kwa usiku mmoja. Kamwe usidanganywe na matangazo ya kuwa utafanywa kuwa tajiri mkubwa siku moja. Mambo hayaendi hivyo.

Awali ya yote utahitaji kuwa na blog yako; pia utahitajika kuwekeza rasilimali ya muda au pesa kiasi fulani ili kuweza kuona matokeo kutokana na blog yako.

1. Kuwa wakala

Unaweza kupata pesa kwenye blog yako kwa njia ya kuwa wakala wa wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mara mtu anunuapo kitu kwa kukifikia kupitia blog yako basi utapata gawio.

Unaweza kujiunga na huduma hizi ili kuwa wakala:
Amazon
Commission Junction
ShareASale
Baada ya kuchagua bidhaa ya kuitangaza unaweza kutumia ThirstyAffiliates kutawala matangazo hayo.

2. Jiunge na Google Adsense

Kama una watembeleaji wengi kwenye blog yako kuanzia 1,000 au zaidi kwa siku, unaweza kujiunga na huduma hii na ukapata pesa kutokana na matangazo yatakayowekwa na Google kwenye blog yako.

Aina za utangazaji wa Google Adsense:
CPC – Cost Per Click ni matangazo ambayo utalipwa kadri watumiaji wa blog yako wanavyobofya au kuclick tangazo husika. Kiwango cha malipo kwa click hutegemea kiwango kilichowekwa na mtangazaji.
CPM – Cost Per Thousand impressions ni matangazo ambayo utalipwa kutokana na tangazo kuonwa mara 1,000.

3. Njia ya kuweka matangazo moja kwa moja

Unaweza kukubaliana na kampuni husika moja kwa moja kuweka tangazo lao kwenye nafasi fulani ya blog yako. Kwa njia hii unaweza kupata pesa zaidi kuliko kutumia huduma nyingine ambazo ndizo hukubaliana na makampuni husika au mtangazaji.

4. Andika posti iliyodhaminiwa

Hii ni post inayoandikwa kwa lengo la kufafanua au kutangaza huduma au bidhaa fulani. Kampuni husika itakulipa kwa kuandika post inayoelezea na kutangaza bidhaa au huduma yao.

5. Uza blog

Kuuza blog? Ndiyo, kuuza blog kunaweza kukupatia kipato kizuri kabisa. Kama unajua kusanifu na kutengeneza blog, basi unafahamu kitu cha ziada. Kuna watu wengi wanahitaji kununua blog zilizotengenezwa tayari. Unaweza kutafuta anwani nzuri (domain) na kuitengenezea blog kisha ukaiuza kupitia tovuti kama vile Flippa na kujipatia pesa.

6. Tengeneza maudhui ya wanachama

Unaweza ukatengeneza maudhui kwenye blog yako ambayo yanaweza kufikiwa na wanachama waliojisajili tu. Unaweza kupata pesa kwa njia ya kuwatoza ada ya usajili au uwanachama wale wote wanaohitaji kujisajili kwenye blog yako. Kwa njia hii utajipatia kipato moja kwa moja kutokana na wanachama watakaojisajili ili kusoma maudhui hayo.

7. Uza vitabu pepe

Kama una maarifa fulani unaweza kuyaweka kwenye mfumo wa vitabu pepe (e-books) na kuuza vitabu hivyo ili kujipatia pesa. Unaweza ukatengeneza kitabu chako katika mfumo wa PDF na kuwatoza watu kiasi fulani cha pesa ili kuweza kukipakua kama ninavyofanya mimi. Bonyeza hapa uone KITABU: MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI

8. Uza kozi za kwenye mtandao

Kama ilivyo kwenye swala la vitabu, unaweza pia ukandaa kozi za kuwafundisha watu mambo mbalimbali unayoyafahamu. Andaa kozi vizuri na kwa ubora, zitangaze kwenye blog yako na watu wanaweza kujiunga kwa kulipa ada fulani ambayo itakupatia pesa kama ambavyo mimi ninafanya. Bonyeza hapa uone. PIUS ONLINE COLLEGE

9. Tafuta kazi kwa kuuza ujuzi wako

Kama una ujuzi wa kufanya kazi au jambo fulani unaweza kutumia blog yako kujitangaza na ukajipatia kipato cha kutosha. Watu wanapotembelea blog yako wanaweza kuvutiwa na ujuzi wako hivyo wakakuajiri ili uwafanyie kazi fulani.

10. Kuwa mshauri au kocha

Kama unauwezo wa kuwashauri watu au kuwahamasisha juu ya maswala mbalimbali ya maisha, unaweza kutumia blog yako kufikia wateja wako. Unaweza ukawahudumia kupitia mtandao au ukawaalika moja kwa moja ofisini kwako. Maswala haya yanaweza kuwa tiba, mahusiano, elimu, uchumi, malengo, maono n.k. Unaweza kuwatoza gharama fulani kutokana na huduma husika na ukajipatia pesa.

11. Anza duka la kwenye mtandao

Kama unatumia WordPress kwenye blog yako unaweza kutumia WooCommerce pluginkuanzisha duka la kwenye mtandao na ukauza bidhaa mbalimbali. Kwa njia hii unaweza kuuza bidhaa zako au za watu wengine na ukajipatia kiasi kizuri cha pesa.

12. Uza mavazi yenye chapa yako

Kama unachapa (brand) maarufu ama ya blog au kampuni yako unaweza kuitumia kuuza mavazi na ukajipatia pesa. Unaweza kuuza mavazi yenye chapa yako kama vile tisheti, kofia, mikanda, bangili, mikoba, viatu n.k kupitia blog yako.

13. Uza kazi ya usanifu mtandao

Kama unajua kutengeneza plugins za wordpress, extension za Joomla, violezo (themes/templates) n.k unaweza kuvizua kupitia blog yako na ukajipatia kiwango kizuri cha pesa.

14. Pokea msaada

Hii ni njia ambayo si maarufu sana lakini inaweza kukuwezesha kupata pesa. Umewahi kufikiri tovuti kama wikipedia inajiendeshaje? Inajiendesha kwa kutegemea michango ya misaada ya wasomaji wake. Kama unatoa maarifa au huduma fulani nzuri bila malipo kwanini usiombe msada kwa mtu anayependa kufanya hivyo? Unaweza ukapata kiwango kizuri cha fedha kupitia njia hii.

Hitimisho

Naamini umeweza kufunguka macho na kuona fursa ambazo hukuwa umeziona ua kuzielewa vyema mwanzoni. Ni vyema ukafahamu kuwa hakuna njia ya mkato kupata pesa. Ni vyema ukajitahidi kufanya bidii na kuwekeza muda au fedha kiasi fulani kwenye blog yako ili uweze kujipatia kipato kizuri.

Kama utapenda kuanza kutengeneza jina lako na hatimaye uanze kutengeneza kipato chako kupitia blog wasiliana nasi tuweze kukutengenezea blog simple na nzuri itakayoweza kukutengenezea jina na uaminifu kwa wasomaji wako na hatimaye kukuingizia kipato kikubwa.

Wasiliana nasi kwa whatsapp 0754745798. KARIBU SANA.

Kama umependa makala hii na ungependa kupata makala kama hizi basi download PIUS JUSTUS APP na uweze kupata notification kila mara. Bonyeza hapa chini kudownload moja kwa moja.



Asante kwa kusoma makala haya.
Ni mimi ninayejali mafanikio yako;

Pius J. Muliriye
075474578 | Whatsapp only.

Tuesday, January 16, 2018

JINSI YA KUPATA KITABU CHA MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI KWA BEI RAHISI SANA

Habari rafiki,

Leo hii nimekuletea njia rahisi sana ambayo itakusaidia kupata kitabu chako kwa njia rahisi kabisa na kwa bei nafuu kabisa.
sikiliza video hii na uchukue hatua kama hujapata copy yako.


Saturday, October 7, 2017

PATA FAIDA KWA KUTENGENEZA NA KUUZA MAFUTA YA NAZI

Habari rafiki yangu na mfatiliaji wa mtandao huu wa shuletanzania.
Katika mfululizo wa makala zangu za kukuonyesha ni product gani zinazotengenezwa kwa njia rahisi na kutengeneza pesa nyingi.

Nimekufundisha kuhusu mambo mengi hasa kupitia channel yangu ya yutube, unaweza kuangalia kama hujafanikiwa kuona video hiyo.

Leo nakushirikisha kuhusu mgodi mwingine ambao bado watu hawajaujua sana na wale wanaoujua hawajajua watafanyaje ili kupata ubora na jinsi gani waingie sokoni.

Bidhaa hiyo ni MAFUTA YA NAZI. Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri sana kwa kupikia na hata kwa kupaka kwenye ngozi kwa afya ya ngozi yako.












Mafuta haya yana soko kubwa sana, na mengi yanatoka kenya na wakati Tanzania tunalima nazi hasa kwa watu wa dar es salaam.

Ndani ya kitabu changu ambacho kinafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zaidi ya 15 nimekuwekea pia jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi kwa njia rahisi sana na kupata mafuta yenye ubora wa hali ya juu sana.

Ndani ya kitabu hicho utajifunza kukamua mafuta ya nazi kwa njia ya haraka na kupata mafuta mengi sana kwa kutumia mashine ndogo ambayo watu wengi hawajui kabisa. Na ninakuhakikishia inaweza kukuweka sokoni kwa muda mrefu na kutengeneza pesa bila kikomo. Pia nimekuwekea mawasiliano na viwanda vinavyotengeneza vifungashio ili uweze kupata vifungashio vya bidhaa yako kwa njia rahisi sana.

Jipatie kitabu hicho kwenye simu yako ili uchukue hatua mara moja na uanze biashara hii. Pia utaona aina hii ya mashine na bei yake. Mashine hii inakamua mafuta ya mbegu kama karanga, zaituni, mbegu za maboga na hata alizeti, kwahiyo ina faida kubwa sana kibiashara.

Fikiria nje ya box na watu watabaki wanakushangaa.
Kitabu hicho kipo kwenye mfumo wa softcopy yaani nakala laini ambapo unaweza kukisoma kwenye simu yako au kompyuta yako. Na unaweza kukipata kwa njia ya mbili.

1. Moja kwa moja kutoka kwangu kwa kutuma pesa ya kitabu sh. 5000/- kwa MPESA 0754745798-Pius au TIGOPESA 0657128567-Pius nami nitakutumia kitabu kwa njia ya Email au whatsapp.

2. Unaweza kukipata moja kwa moja kupitia mtandaoni kwa kubonyeza HAPA na utaweza kukidownload au kukipakua kwa bei hiyo hiyo.

Asante kwa kusoma makala hii. Chukua hatua mara moja na unufaike katika maisha yako.

Kama hujajiunga na huduma zetu basi unaweza kujiunga hapa chini ili uwe karibu na huduma tunazozitoa kwa njia ya email;



Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako.

Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

JIUNGE NAMI UPOKEE MAKALA KILA IWEKWAPO MTANDAONI