0657128567

Mwanza Tanzania,

Karibu Sana Kwenye Mtandao huu Wa Shule Tanzania

Showing posts with label HAMASIKA. Show all posts
Showing posts with label HAMASIKA. Show all posts

Friday, July 27, 2018

DON'T WAIT UNTILL THINGS GET READY!

Nilikutana na huyu mtu James mwang'amba back 2009, alikuwa akifundisha somo la self development kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na nilipata bahati ya kuhudhuria mafundisho yake kwa siku 2 mfululizo!



Alizungumza kitu ambacho kili stick katika kichwa changu ambapo alisema USISUBIRI MPAKA MAMBO YAWE SAWA KUPIGANIA NDOTO ZAKO!!

Kwa mara ya kwanza sikumuelewa kabisa, kwa sababu nilikuwa nikifikiria huwezi kufanikiwa ukiwa katika nchi maskini kama Tanzania, huwezi kufanya lolote bila serikali kukutengenezea mazingira, na nilikuwa miongoni mwa watu wanaolalamika sana nikiona mambo hayaendi sawa!
.
.
Baada ya miaka mitatu wakati napitia makablasha yangu nikakutana na notebook niliyoandika masomo aliyokuwa akifundisha, nikakutana na sentensi hiyo tena iliyokuwa ikisema " Don't wait untill this get ready"...

Hapo ndipo nilipoanza kujitafuta mimi ni nani!

Siku hiyo nilipata wazo la kuandika kitabu ili niweze kushea na watanzania ujuzi nilionao na niliamini kabisa kitabu changu kingewasaidia wengi!

Nilimshirikisha rafiki yangu nikamwambia nataka niandike kitabu hiki ninaamini kitauzika sana na watu watanufaika na mimi nitanufaika pia, alicheka sana akaniambia hivi wewe unawajua watanzania???? Tangu lini watanzania wakawa wasomaji wa vitabu?? Nakuhakikishia hutauza kitabu hata kimoja unapoteza muda na nguvu zako achana na wazo hilo, kwanza gharama za kuzalisha kitabu hicho ziko juu sana hutaweza kabisa.😒

Kusema ukweli alinikatisha tamaa, nikaanza kuwaza upya juu ya maoni yake, lakini nikakumbuka kabisa mwalimu wangu James Mwang'amba aliniambia kijana "Usisubiri kabisa mambo yawe sawa ndio uchukue hatua" ndipo nilipojiambia sitasubiri mpaka watanzania wapende kusoma vitabu ndipo niandike.....!! Nikaanza mara moja kuandika na nikakamilisha kitabu changu ndani ya mwezi mmoja!

Shida nyingine ikaja, Sina pesa ya kupublish kitabu changu pamoja na kuzalisha copy nyingi na kusambaza, nikakwama na nikaacha na kuendelea na mambo mengine!!
.
.
Lakini mwaka 2017 mwezi wa kwanza nikapata wazo ambalo lilinifanya nishindwe kulala kabisa, nikakumbuka kuwa nina simu ya smartphone, nima laptop ambayo nilinunua wakati nipo chuo kikuu lakini vikawa havinisaidii chochote, ndipo nilipoanza kuvitumia na kuanza kusoma wenzetu nchi za nje wanafanya nini!..

Nikapata mwanga na nikaanza sasa kufanyia kazi elimu ile niliyoipata na mwaka huo huo mwezi wa nne nikafanikiwa kufungua channel yangu ya Youtube na nikarekodi video yangu ya kwanza kwa kutumia simu yangu ya mkononi nikizungumzia kitabu changu na faida zake na kukitangaza kwa atakayehitaji kupata ujuzi huo nitamtumia kwenye whatsapp au email yake.....Sikuamini macho yangu😀😀😀

Nilipata oda nyingi sana, na sasa video ile ina views zaidi ya 20,000 na nimeshauza copy takribani 3650 mpaka sasa bila gharama ya kutoa copy wala usambazaji, copy zote nimetuma nikiwa ndani kwangu, kwenye gari nikiwa nasafiri, nikiwa kijiweni napiga story na marafiki zagu n.k. hii ndio nguvu ya TEKNLOJIA, wewe unatumiaje mapinduzi haya ya teknolojia??

Siku hizi watu hawahangaiki kufanya malipo MPESA, TIGOPESA n.k ziko kila mahali mtu akipenda kitu hasumbuki kulipia, tumia nafasi hiyo utafanikiwa.

Nakushauri wewe kijana mwenzangu, mazingira yasikifanye ushindwe kupigania ndoto yako, usisubiri serikali itengeneze mazingira ya biashara ndipo ufanye, wakati huo fursa itakuwa si yako tena, isome jamii yako ina matatizo gani kisha tafuta jawabu la matatizo yao na maisha yako yatabadilika.

Asanteni sana na niwatakie siku njema!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Pius J. Muliriye
www.piusjustus.com

Friday, February 16, 2018

FANYA HIVI KUGUNDUA KIPAJI CHAKO.

Moja ya changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni kutojua kwa undani kipi  kipaji chako ambacho Mungu amekupa na ambacho unaweza ukakitumia kwa namna moja ama nyingine ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika jamii na wewe binafsi.


Na kwa kuwa kuna watu wengi ndio wapo kundi hilo, kuna usemi unasema ya kwamba wengi wape basi ngoja nifanye hivyo kuweza kuwapa somo hilo la namna ya kujua kipaji chako  kwani hii itamsadia kila mmoja ambaye atakwenda kufuatana nami mwanzo hadi mwisho katika mukutadha wa makala haya.
Tunapozungumzia neno kipaji huenda kila mmoja akawa na maana yake ambayo anaifahamu, lakini kwa namna moja ama nyingine ni lazima mtu aweze kuzaliwa nacho hivyo Mwenyezi Mungu huhusika pia katika kumpa mtu kipaji.
Hivyo endapo mtu atakifahamu kipaji chake inampasa sasa ajue namna ya kukiendeleza kipaji hicho ili kisife. Pia ikumbukwe ya kwamba tunapozungumzia kipaji tunamzungumzia binadamu na maisha yake kwa ujumla.
Katika tafiti ambazo zimewahi fanywa na  Dr. Fred Luskin kutoka Stanford university yeye aliweza kugundua ya kwamba asilimia 65 ya watu wengi hawajui vipaji vyao na katika kundi kubwa la idadi hii ya watu ndio ambao wanafanya vitu ambavyo sio vyao.
Na pia  asilimia 35 iliyobaki hawa ndio ambao wameweza kuvijua hivyo vipaji vyao ingawa haviwasadii katika maisha yao na wengine kwa asilimia 100, hii ni kutoka mafanikio yatokanayo vipaji hivyo huwa ni ya muda mrefu.
Hivyo kwa kuwa watu wengi tunataka mafanikio ya muda mfupi uvumilivu hufika ukomo na kujikuta tunaviacha vitu hivyo na kuingia kufanya vitu vingine.
Mfano mtu anakuwa na kipaji cha kucheza mpira katika timu kubwa hapa nchini na nje ya nchi,na kwa kuwa huenda amecheza kwa muda mrefu bila matarajio yake kutimia mtu huyo huacha kile ambacho hukifanya na kuamua kufanya kitu kingine ambacho sio kipaji chake mwishowe mtu huyo anajikuta anafanya hiki anakiacha mara kile nacho anakiacha.
Ukiona hicho unachokiita kipaji chako hakitoi burudani, hakifundishi, hakishangazi basi hicho sio kipaji.
Namna ya kugundua kipaji chako.
  1. Kumuomba Mungu.
Hapa huwa pananifanya nimkumbuke sana rafiki yangu Samweli Salali kwani aliwahi kuniambia ya kwamba kipaji ni kusudio la Mungu kwa kila mja wake. Kwani katika mafundisho yake katika vitabu vya dini vinasema kabla sijaumba nilikujua.
Hii inamaana kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ana kipaji chake, hivyo kinauwezo mkubwa wa kubadili maisha yake na jamii kwa ujumla, ila kipaji hicho watu wengi hawahujui mpaka dakika hii kuwa kipi kipaji chake ambacho Mungu kampa.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwa watu hao ni muda wako muafaka wa kutumia Muda huu kumuomba Mungu akuonyeshe kipaji chako hasa na kipi kwa sasa?

  1. Marafiki, ndugu na wazazi.Hili ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kipaji chako. Labda unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao wanakuzunguka ndio wana picha kamaili juu ya maisha yako.
Kwa mfano mtu akiwa mlevi hawezi kusema mimi ni mlevi ila watu ambao wanakuzunguka ndio ambao watasema yule jamaa ni mlevi sana. Picha hiyohiyo ya kumuona mtu mwingine tabia yake ndiyo ambayo inatumika kujua kipaji chako.
Hebu waulize nyie mnanionaje, mna picha gani? Mnahisi nina kipaji Gani? Baada ya kuwauliza hayo wao ndio watakupa picha kamili juu ya kipaji chako na maisha yako kwa ujumla.

3. Matatizo.
Matatizo ni njia nzuri ya bora sana ya kugundua kipaji chako. Ulimwegu wa leo ni ulimwengu wenye changamoto nyingi sana, hata hivyo kutokana na suala hilo, pale matatizo yanapotokea na kuyapatia ufumbuzi sahihi hapo ndipo utakapojua kipaji chako.
Kwa mfano watu wengi leo hii wanapenda maisha ya kufanyiwa kila kitu. Tuchukulie leo hii unamtegemea mtu fulani ili aweze kukutimizia lengo lako. Halafu siku ya siku mtu huyo anakufukuza nyumbani kwake na kukuambia nenda kajitegemee.
Baada ya kuambiwa hivyo ndipo unakuja kugundua ni kipi kipaji chako baadala ya kuendelea kuwa tegemezi. Hebu tuone mfano mwingine unakuta mtu alikuwa ni mfanyakazi wa ofisini ila baada ya kustafu unajikita katika ufugaji mwisho wa siku unagundua wewe ulikuwa una kipaji cha ufugaji badala ya kufanya kazi za maofisini.
Hivyo wito wangu kwako ni vyema ukagundua kipaji chako mapema usisubiri changamoto fulani zitokee ndipo ugundue kipaji chako.
  1. Mashindano.
Kuna baadhi ya nchi huandaa mashindano mbalimbali kwa ajili ya kusaka vipaji, hili jambo jema sana hata hapa kwetu nchini kuna baadhi ya mashindano hufanyika ambayo husaidia kujua vipaji vya watu kama vile bongo star search, fiesta, DJ compition, umiseta na mangineyo mengi.
Hivyo kama kweli unataka kujua kipaji chako endapo yatatokea mashindano yoyote yale jitahidi sana kwenda kushiriki kwani hii itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kujua ni kipi kipaji chako.
Mpaka kufikia hapo niweke nukta kwa kusema kama ukwisha kugundua hicho kipaji chako ni vyema ukajua ni namna gani ya kugeuza hicho kipaji chako kuwa pesa, kwani hapo ndipo palipo kuwa na changamoto kubwa.

Sunday, February 11, 2018

Njia 14 Halali za Kupata Pesa Kupitia Blog

Je unatafuta njia ya kujipatia pesa kwenye mtandao ambayo siyo ya utapeli? Blog ni njia moja wapo unayoweza kuitumia kujipatia fedha huku ukifanya kile ukipendacho. Katika makala hii nitakushirikisha njia 14 unazoweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia blog yako.



Kumbuka! Hizi si njia za kupata pesa za mteremko haraka haraka kwa usiku mmoja. Kamwe usidanganywe na matangazo ya kuwa utafanywa kuwa tajiri mkubwa siku moja. Mambo hayaendi hivyo.

Awali ya yote utahitaji kuwa na blog yako; pia utahitajika kuwekeza rasilimali ya muda au pesa kiasi fulani ili kuweza kuona matokeo kutokana na blog yako.

1. Kuwa wakala

Unaweza kupata pesa kwenye blog yako kwa njia ya kuwa wakala wa wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mara mtu anunuapo kitu kwa kukifikia kupitia blog yako basi utapata gawio.

Unaweza kujiunga na huduma hizi ili kuwa wakala:
Amazon
Commission Junction
ShareASale
Baada ya kuchagua bidhaa ya kuitangaza unaweza kutumia ThirstyAffiliates kutawala matangazo hayo.

2. Jiunge na Google Adsense

Kama una watembeleaji wengi kwenye blog yako kuanzia 1,000 au zaidi kwa siku, unaweza kujiunga na huduma hii na ukapata pesa kutokana na matangazo yatakayowekwa na Google kwenye blog yako.

Aina za utangazaji wa Google Adsense:
CPC – Cost Per Click ni matangazo ambayo utalipwa kadri watumiaji wa blog yako wanavyobofya au kuclick tangazo husika. Kiwango cha malipo kwa click hutegemea kiwango kilichowekwa na mtangazaji.
CPM – Cost Per Thousand impressions ni matangazo ambayo utalipwa kutokana na tangazo kuonwa mara 1,000.

3. Njia ya kuweka matangazo moja kwa moja

Unaweza kukubaliana na kampuni husika moja kwa moja kuweka tangazo lao kwenye nafasi fulani ya blog yako. Kwa njia hii unaweza kupata pesa zaidi kuliko kutumia huduma nyingine ambazo ndizo hukubaliana na makampuni husika au mtangazaji.

4. Andika posti iliyodhaminiwa

Hii ni post inayoandikwa kwa lengo la kufafanua au kutangaza huduma au bidhaa fulani. Kampuni husika itakulipa kwa kuandika post inayoelezea na kutangaza bidhaa au huduma yao.

5. Uza blog

Kuuza blog? Ndiyo, kuuza blog kunaweza kukupatia kipato kizuri kabisa. Kama unajua kusanifu na kutengeneza blog, basi unafahamu kitu cha ziada. Kuna watu wengi wanahitaji kununua blog zilizotengenezwa tayari. Unaweza kutafuta anwani nzuri (domain) na kuitengenezea blog kisha ukaiuza kupitia tovuti kama vile Flippa na kujipatia pesa.

6. Tengeneza maudhui ya wanachama

Unaweza ukatengeneza maudhui kwenye blog yako ambayo yanaweza kufikiwa na wanachama waliojisajili tu. Unaweza kupata pesa kwa njia ya kuwatoza ada ya usajili au uwanachama wale wote wanaohitaji kujisajili kwenye blog yako. Kwa njia hii utajipatia kipato moja kwa moja kutokana na wanachama watakaojisajili ili kusoma maudhui hayo.

7. Uza vitabu pepe

Kama una maarifa fulani unaweza kuyaweka kwenye mfumo wa vitabu pepe (e-books) na kuuza vitabu hivyo ili kujipatia pesa. Unaweza ukatengeneza kitabu chako katika mfumo wa PDF na kuwatoza watu kiasi fulani cha pesa ili kuweza kukipakua kama ninavyofanya mimi. Bonyeza hapa uone KITABU: MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI

8. Uza kozi za kwenye mtandao

Kama ilivyo kwenye swala la vitabu, unaweza pia ukandaa kozi za kuwafundisha watu mambo mbalimbali unayoyafahamu. Andaa kozi vizuri na kwa ubora, zitangaze kwenye blog yako na watu wanaweza kujiunga kwa kulipa ada fulani ambayo itakupatia pesa kama ambavyo mimi ninafanya. Bonyeza hapa uone. PIUS ONLINE COLLEGE

9. Tafuta kazi kwa kuuza ujuzi wako

Kama una ujuzi wa kufanya kazi au jambo fulani unaweza kutumia blog yako kujitangaza na ukajipatia kipato cha kutosha. Watu wanapotembelea blog yako wanaweza kuvutiwa na ujuzi wako hivyo wakakuajiri ili uwafanyie kazi fulani.

10. Kuwa mshauri au kocha

Kama unauwezo wa kuwashauri watu au kuwahamasisha juu ya maswala mbalimbali ya maisha, unaweza kutumia blog yako kufikia wateja wako. Unaweza ukawahudumia kupitia mtandao au ukawaalika moja kwa moja ofisini kwako. Maswala haya yanaweza kuwa tiba, mahusiano, elimu, uchumi, malengo, maono n.k. Unaweza kuwatoza gharama fulani kutokana na huduma husika na ukajipatia pesa.

11. Anza duka la kwenye mtandao

Kama unatumia WordPress kwenye blog yako unaweza kutumia WooCommerce pluginkuanzisha duka la kwenye mtandao na ukauza bidhaa mbalimbali. Kwa njia hii unaweza kuuza bidhaa zako au za watu wengine na ukajipatia kiasi kizuri cha pesa.

12. Uza mavazi yenye chapa yako

Kama unachapa (brand) maarufu ama ya blog au kampuni yako unaweza kuitumia kuuza mavazi na ukajipatia pesa. Unaweza kuuza mavazi yenye chapa yako kama vile tisheti, kofia, mikanda, bangili, mikoba, viatu n.k kupitia blog yako.

13. Uza kazi ya usanifu mtandao

Kama unajua kutengeneza plugins za wordpress, extension za Joomla, violezo (themes/templates) n.k unaweza kuvizua kupitia blog yako na ukajipatia kiwango kizuri cha pesa.

14. Pokea msaada

Hii ni njia ambayo si maarufu sana lakini inaweza kukuwezesha kupata pesa. Umewahi kufikiri tovuti kama wikipedia inajiendeshaje? Inajiendesha kwa kutegemea michango ya misaada ya wasomaji wake. Kama unatoa maarifa au huduma fulani nzuri bila malipo kwanini usiombe msada kwa mtu anayependa kufanya hivyo? Unaweza ukapata kiwango kizuri cha fedha kupitia njia hii.

Hitimisho

Naamini umeweza kufunguka macho na kuona fursa ambazo hukuwa umeziona ua kuzielewa vyema mwanzoni. Ni vyema ukafahamu kuwa hakuna njia ya mkato kupata pesa. Ni vyema ukajitahidi kufanya bidii na kuwekeza muda au fedha kiasi fulani kwenye blog yako ili uweze kujipatia kipato kizuri.

Kama utapenda kuanza kutengeneza jina lako na hatimaye uanze kutengeneza kipato chako kupitia blog wasiliana nasi tuweze kukutengenezea blog simple na nzuri itakayoweza kukutengenezea jina na uaminifu kwa wasomaji wako na hatimaye kukuingizia kipato kikubwa.

Wasiliana nasi kwa whatsapp 0754745798. KARIBU SANA.

Kama umependa makala hii na ungependa kupata makala kama hizi basi download PIUS JUSTUS APP na uweze kupata notification kila mara. Bonyeza hapa chini kudownload moja kwa moja.



Asante kwa kusoma makala haya.
Ni mimi ninayejali mafanikio yako;

Pius J. Muliriye
075474578 | Whatsapp only.

Thursday, February 8, 2018

HII NDIO BIASHARA INAYOLIPA KULIKO ZOTE

Habari rafiki,
nimekuwa nikiulizwa ni biashara gani ambayo ninaweza kumshauri mtu afanye ambayo inalipa sana kuliko zote, na hili ndio jibu sahihi, chukua muda kutazama video hii.

Wednesday, February 7, 2018

MATATIZO YAKO YAWE CHANGAMOTO YAKO


Monday, February 5, 2018

EIMU NA UHALISIA WA MAISHA


Profesa wa Chuo kikuu cha Makelele nchini Uganda, aliwambia wanafunzi kuwa:
Mafanikio ya kielimu hayana uhalisi katika maisha. Niliyasema haya:

Kuwa mtu wa kwanza darasani kwako hakuamanishi wewe utafanikiwa kimaisha.

Unaweza kumaliza chuo kama mtaalamu wa fedha au uwekezaji na haiamanishi kwamba wewe utapata au utakuwa fedha nyingi kuliko wengine. Mwanafunzi mwenye ufaulu na shahada ya hali ya juu katika kitivo cha sheria haiamanishi kwamba ndio atakuwa mwanasheria bora.

Ukweli ni kuwa maisha yanahitaji zaidi ya kuelewa nadharia ya masomo, kuyakumbuka na kuyaandika tena kwenye mitihani. Shule zinawazawadia wanafunzi kwa uwezo wao wa kukumbuka. Maisha yanawazawadia watu kwa uwezo wa kiuvumbuzi na ubunifu. Shule zinawazawadia watu kwa uwezo wao wa kuwa waangalifu, maisha yanawazawadia watu kwa uwezo wa kuthubu ka maarifa.
Shule zinawasifia wale wanaoishi kwa kufuata kanuni na sheria. Maisha yanawasifia wale wanaovunja sheria na kanuni zilizotengenezwa katika mtazamo wa kujikwamua kwa vipato halali.

*Kwahiyo naamanisha watu wasisome kwa bidii shule?*

*Lahasha, hapana siamanishi hivyo unatakiwa kusoma kwa bidii*. Lakini usiache kila kitu kikakupita kwasababu ya kupata daraja la kwanza la ufaulu.Usijiwekee mipaka darasani tu. *Pia fanya vitu kwa vitendo vya kimaisha kutokana na elimu yako*
Pata nafasi ya Kiungozi. Anzisha biashara na ushindwe.Hili ni somo zuri la biashara la 101.Jiunge au anzisha klabu. Jaribu kugombea nafasi ya Kisiasa ili ushindwe. Itakufundisha kitu katika somo la Siasa 101 ambalo usingejigunza.Hudhuria mijadala na mafunzo. Soma vitabu nje ya mtaala wa masomo yako. Nenda katika safari na shinda katika kupata ya nje....Fanya kitu unachoamini. Fikiria zaidi kuwa mtu bora na sio kuwa mwanafunzi bora.

Usifanya darasa kuwa dunia yako bali dunia kuwa darasa lako. Nenda mbele, Jaribu siasa, Jaribu kilimo,Jaribu biashara, Jaribu na kitu kingine.
Na Mungu atakujalia

*Umeipenda?*
 tafadhali watumie na wengine wajifunze.

Wednesday, January 31, 2018

Hatua Tano Muhimu Za Kufikia Malengo Uliyojiwekea

Hizi Ndizo Hatua Tano Muhimu Za Kufikia Malengo Uliyojiwekea.


Habari rafiki, karibu katika makala nyingine ambayo tutazungumzia hatua 5 muhimu za kukusaidia wewe kufikia malengo yako uliyojiwekea. Ninatambua kila mwaka huwa unaweka malengo makubwa sana lakini huyafikii kwa sababu mbalimbali. Nimekuwekea hatua 5 za kupitia ili uweze kutimiza ndoto zako, twende pamoja.


1. Ni lazima uwe na hamasa ya kutaka kufanikiwa.

Hautaweza kufanikiwa kama huna njaa na kiu kubwa ya mafanikio ndani mwako. Ili uweze kufanikiwa hasa kwa malengo uliyojiwekea ni lazima uwe na hasira kubwa ya mafanikio. Ukiwa na hasira hii, itakusaidia wewe kupita eneo lolote, hata katikati vizuizi ama vikwazo ambavyo huwa tunakutana navyo katika safari ya mafanikio. Watu wengi wenye mafanikio makubwa duniani ni watu ambao walikuwa na hasira na malengo yao waliyojiwekea. 
 
2. Anza kuchukua hatua mapema.

Kuongea sana juu ya mipango na malengo mazuri uliyonayo hakutakusaidia kitu, zaidi ya kuchukua hatua muhimu za kuelekea kwenye utekelezaji. Anza kuchukua hatua mapema za kutekeleza ndoto zako hata kwa kidogo kidogo ipo siku utafika. Ni bora ukafanya kwa kidogo hiyo itakusaidia sana tofauti na ambavyo ungekaa na kusubiri, hiyo ingekuwa inakupotezea muda sana katika maisha yako.

3. Unahitaji kujifunza zaidi.

Hii ni hatua muhimu pia ya kufikia malengo unayoyahitaji katika maisha yako. Ni muhimu kujifunza na ukapata maarifa yanayoendana na malengo unayoyahitaji katika maisha yako. Hiyo itakusaidia kujua vitu vya msingi vinavyoendana na malengo uliyojiwekea. Kwa mfano, kama malengo yako ni kuwa millionea baada ya miaka 20 kuanzia sasa ni lazima uanze kujifunza kuishi maisha wanayoishi mamilionea kwa kujisomea kila siku.

4. Unahitaji kuwa na mitazamo chanya.

Mara nyingi kuna wakati huwa tunashindwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kutokana na mitazamo tuliyonayo juu ya malengo yetu. Kama unajiona huwezi kufikia malengo yako, huo ndio ukweli hutaweza kuyafikia. Jenga mitazamo chanya ambayo itakusaidia kufikia malengo muhimu uliyojiwekea. Achana na fikra ama imani za kuwa huwezi kufanikiwa kwa sababu hii na hii, jiwekee mitazamo chanya na utaweza kufikia malengo yako.

5. Jifunze kutokana na makosa.

Kuna wakati huwa tunafikia mafanikio kwa yale tunayoyahitaji baada ya kukosea sana hiki na kile. Hautaweza kufikia mafanikio au malengo yako kwa urahisi kama unavyofikiri, kuna wakati ni lazima ukosee. Unapokosea huo ndio huwa wakati muhimu kwako wa kujifunza kutokana na makosa uliyoyafanya.  Acha kusononeka wala kulia kama kuna sehemu umekosea, hiyo hatakusadia kitu. Badala yake, chukua hatua muhimu ya kunyanyuka pale ulipoanguka, jifunze na kisha songa mbele.

Mwisho, unaposhindwa kufikia malengo yako kwa namna yoyote ile acha kulaumu vitu ambavyo viko nje ya wewe kuwa ndiyo vimesababisha ushindwe kufikia malengo uliyojiwekea. Mara nyingi sisi wenyewe huwa ndio huwa vizuizi wa malengo yetu. Jifunze hatua hizo tano muhimu zikusaidie kufikia malengo muhimu uliyojiwekea katika maisha yako.

Asante sana kwa kusoma makala haya. kwa mawasiliano zaidi au kama unahitaji ushauri kwa kitu chochote kile niandikie whatsapp 0754745798.

Download PIUS JUSTUS APP ili uweze kuwa karibu na makala haya kila siku. Bonyeza hapa chini kudownload APP hiyo


Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

Pius Justus Muliriye
0754745798-whatsapp



HII NDIO AKILI YA USHINDI


Hakuna mtu ambaye ni mkamilifu katika maisha yake, na haimaanishi wewe kutokuwa mkamilifu huna cha kumsaidia wengine.Kila chenye pungufu kina sehemu flani ambayo ni lulu katika maisha yake na ya wengine.

 Usidhani mtu kuwa na mapungufu Mungu hawezi kukuona na kukutumia kufanya mambo makubwa. Nikupe mfano mmoja wa Zakayo mtu mfupi aliyekuwa mtoza ushuru na mtenda dhambi,unadhani Zakayo angelalamikia ufupi wake katika makutano ya watu angeweza kupanda mti na kumwona Yesu, unadhani angelalamika kuhusu dhambi zake hata angethubutu kuwa na kiu ya kumwona Yesu.

Lakini sasa tazama ilivyoajabu kwamba licha ya mapungufu yake na wingi wa watu waliokuwa wakimfuata Yesu kiu aliyokuwa nayo Zakayo licha ya kuwa mtu wa dhuluma lakini Yesu aliweza kugeuka na kumwita na kumwambia kwamba atakuwa mgeni nyumbani kwake kushiriki nae chakula (spiritual connection).

 Ufupi wa Zakayo ni mapungufu yako,ufupi wa Zakayo ni matatizo ambayo unapitia,ufupi wa Zakayo ni shida ambazo unakumbana nazo bila kikomo lakini kumbuka ufupi huu usiwe kikwazo cha wewe kudhubutu kama Zakayo aliamua kuthubutu kupanda mti kumwona Yesu hata wewe sasa ni wakati wa kuchukua hatua zaidi ya changamoto zako, sasa ni wakati wa kuwa na Akili Ya Ushindi katika kila jambo ambalo unaligusa ili Mungi aweze kukutumia.

Nikwambie kitu kimoja kwamba Yesu alivyokuwa akichagua mitume wake 12 hakuangalia dhambi walizokuwa nazo naimani alikuwa ndani ya mioyo ya watu na kuamini kwamba kila mmoja anaweza kubadilika na kuwa zaidi ya matendo yake mabaya aliyokuwa akitenda. Wewe na mimi sasa ni wakati wetu wa kutumiwa na Mungu kufanya mambo makubwa yasiyo na kikomo katika maisha yetu.

Nikutakie siku njema;

PIUS J. MULIRIYE
0754745798-WHATSAPP

Sunday, January 28, 2018

STORY YA CHURA KATIKA MAFANIKIO YAKO

*CHURA*


Mchukue chura then muweke kwenye chombo ambacho ni good conductor of heat kikiwa na maji ndani yake,then anza kuchemsha maji akiwemo na chura ndani yake..!

Kadri temperature inavyo ongezeka chura nae huwa ana increase temperature ya mwili wake. pindi temp  inapokaribia kufika boiling point yaani nyuzi 100 chura atashindwa kuongeza temperature ktk mwili wake na hapo ndipo atataka kutoka ktk maji hayo ya moto na yanayo endelea kuchemka!

kutokana na kutumia nguvu nyingi sana ktk kuongeza temperature ktk mwili wake,pindi anapotaka kuruka atashindwa na atakufa humo ndani ya chombo cha maji yanayochemka.

*SWALI;*

*NINI KIMEMUUA CHURA.!??*

Najua utaniambia ni maji ya moto...

La hashaa.!

kilichomuua chura ni kushindwa kufanya maamuzi mapema ya kutoka katika chombo cha maji yanayochemka hali ya kuwa bado nguvu anazo..

*FUNZO*

Fanya maamuzi sahihi sasa kabla nguvu za kutaka kufanya changes hazijakuishia kama yaliyomkuta chura..

*NOTE*

Kuvumilia jambo usiloliweza ni sifa ya Chura.

BADILIKA

Nikutakie siku njema.

Pius J. Muliriye
0754745798

Monday, January 22, 2018

FANYA ILI WAONE ULIVYO TOFAUTI NA WAO

Sunday, January 21, 2018

[AUDIO]: JINSI YA KUTUMIA INTERNET KUFANYA BIASHARA.

NGUVU YA IDEA


KOSA UNALOLIFANYA KATIKA BIASHARA YAKO

Habari rafiki, natumaini uko salama kabisa na unaendelea vizuri na harakati za kuboresha maisha yako.



Leo nahitaji kukupa tip moja muhimu sana katika biashara yako.

Nimekuwa nikisikia watu wengi wakisema biashara zao hazitoki, hazifanyi vizuri sokoni na wengine wamefikia hatua ya kusema biashara zao ni mbaya ndo maana hazinunuliwi.

Leo nataka nikwambie, bidhaa yako ni nzuri sana na jamii inaihitaji sanaaa, tatizo kubwa kwa watu wengi hawajui kufanya masoko (MARKETING).
Nimekuwa nikiona watu wakipost picha za bidhaa zao mtandaoni na bado wanashangaa kwanini watu hawanunui na wakati tangazo lake limeonekana na watu wengi.

Ukitaka kutangaza bishara yako mtandaoni ujue kabisa kuna Formula ambayo inatumika kutangaza biashara mtandaoni na kupata wateja wengi sanaaa.
Siri kubwa ya kufanikiwa mtandaoni jaribu kujifunza sana, acha uvivu, gharamia elimu hiyo utaona matunda yake.

Kama utajitaji nikushike mkono katika kutumia mtandao kufikia watu wengi sana mtandaoni basi wasiliana nami whatsapp 0754745798 tuzungumze na nitakusaidia kufanya hivo.
Asante sana.
Ni mimi ninayejali mafanikio yako.


PIUS J. MULIRIYE
0754745798-Whatsapp

Tuesday, January 16, 2018

JINSI YA KUPATA KITABU CHA MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI KWA BEI RAHISI SANA

Habari rafiki,

Leo hii nimekuletea njia rahisi sana ambayo itakusaidia kupata kitabu chako kwa njia rahisi kabisa na kwa bei nafuu kabisa.
sikiliza video hii na uchukue hatua kama hujapata copy yako.


Monday, January 15, 2018

USHUHUDA WA WALIOJARIBU KUFANYIA KAZI MAFUNZO YA KITABU CHA MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI.

Habari rafiki yangu mpenda maendeleo, naamini uko vizuri na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako.

Leo napenda kukuletea shuhuda za baadhi ya watu ambao wamepata elimu ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani kupitia kwenye kitabu changu cha MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI na wamefanikiwa kutengeneza products hizo na wamenitumia picha za bidhaa zao na kunipongeza kwa kuwasaidia kufikia hatua hiyo.

Picha zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo nimetumiwa, ziangalie na wewe uhamasike kujaribu kutengeneza bidhaa yako, huwezio jua kesho unaweza kutengeneza bidhaa ikawa maarufu na ikawa ndo biashara yako na ikakutoa kimaisha

Asante sana kaka, namshukuru Mungu kupitia kitabu chako nimeweza sasa kutengeneza sabuni ya mche na ina povu jingi sana na imeanza kupendwa sana na watu wanaonizunguka. Nashukuru kwa kunisaidia kupata kazi kwani nimehangaika muda mrefu bila ajira na sasa nimepata cha kufanya naamini itanirahisishia maisha kabisa. Asante sana na Mungu akubariki.

" Kaka nimejaribu kutengeneza sabuni kulingana na maelekezo niliyoyapata kwenye kitabu chako  cha MILIKI KIWANDA na sasa nimeweza kufanya vizuri na nategemea nikirudia nitazidi kufanya vizuri zaidi. asante sana na Mungu akubariki kwa kazi yako ya kuelimisha umaa"
Kaka hii ndo kazi yangu, nimefanikiwa kutengeneza na iko vizuri sana, tatizo liko kwenye kukata sabuni, naomba usichoke kunielekeza, natamani kufanya zaidi ya hapa. Asante sana kwa msaada wako, kitabu chako kimekuwa na msaada mkubwa sana.
Kaka wewe ni mtu hatari sana, natamani watanzania wote wangeweza kujifunza kutoka kwako, umenisaidia sana na sasa ninaanza kuingia sokoni na sabuni yangu imekaa vizuri sana, Mungu akubariki sana ndugu yangu.
 
Kaka nashukuru sana kitabu chako kimenisaidia sana na sasa nimeanzakutengeneza sabuni ya Unga na imetoa povu jingi sana mpaka nimejidharau sana, kumbe mambo haya huwa yanawezekana mtu kutengeneza mwenye we nyumbani, nashukuru sana umenipatia ajira. Mungu akubariki sana Kaka.

Hizo ni baadhi ya shuhuda za watu ambao wamejaribu kufanyia kazi walichokisoma kutoka kwenye kitabu changu cha MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI. 
Naamini siku si nyingi tutakuwa na watu wanamiliki viwanda vyao nyumbani kwao na watakuwa wanatengeneza pesa bila shida kabisa. Kama na wewe ungependa kujifunza ujuzi huo, basi huna budi kupata copy yako ya kitabu hiki, kitakusaidia sana na baada ya hapo tuendelee kuwasiliana ili tuweze kusaidiana pale unapokwama.

kama unapenda kupata kitabu hicho, basi BONYEZA HAPA kukipakua kitabu hicho.

Asante sana na nikutakie siku njema katika kupiga vita umaskini.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;


PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798



Sunday, January 14, 2018

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI ZA MAGADI.

Habari rafiki, nina imani unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako.
Sasa unaweza kujifunza jinsi ya kutengeneza sabuni ya magadi kwa kusikiliza video hii fupi. tafadhari chukua muda na uitazame.

Asante sana, na nikutakie utekelezaji mwema.


Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako.

PIUS JUSTUS MULIRIYE 
0754745798 - Whatsapp

MAMBO MATANO YA KUJUA KABLA YA KUAMUA KUJIAJIRI.

Habari rafiki wa piusjustus.com;

Leo nimekuletea makala kwa njia ya video itakayokufundisha jinsi sahihi ya kujiajiri. Na hays ndio mambo muhimu matano (5) ya kujua kabla ya kuamua kujiajiri.

Karibu usikilize!!





sasa unaweza kupakua app yetu ili uwe wa kwanza kupata makala na video zinapowekwa mtandaoni. Bonyeza hapa kuipakua PIUS JUSTUS APP

Ni mimi mwenye kujalia mafanikio yako;


PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798-whatsapp


Saturday, January 13, 2018

JINSI YA KUWEKA MALENGO YANAYOFIKIKA.

Umbali uliopo kati ya malengo yako na mafanikio ni mrefu sana, na una vikwazo vingi sana, nafahamu fika ya kwamba hilo unalitambua vizuri sana.Umbali huo ambao upo baadhi ya watu ambao wana Mafanikio wameweka mikakati thabiti ambayo imewafanya wameweza kufanikiwa.



Pia kwa upande watu ambao hawajafanikiwa kwa kiwango cha juu na wao katika malengo yao wameweka mikakati, ila wengi wao hukata tamaa njiani katika utekelezaji wa mambo mbalimbali yatayowalete mafanikio.

Hali hiyo hutokea kwa sababu wengi wao hushidwa kuhimili changamoto ambazo hujitokeza katika safari hiyo ya kutoka katika malengo hadi Mafanikio.

Kama na wewe ni miongoni mwa watu ambao hukata tamaa katika safari yako ya kuelekea mafanikio, naomba nichukue nafasi hii kuweza kukaribisha katika makala haya ambapo tutazungumzia masuala ya kupanga malengo yako hadi kufikia mafanikio.

Wengi hujikuta wakishindwa wakiishia njiani katika safari yao ya mafanikio hii ni kutokana kutokujua namna ya kuzitambua mbinu za kukuza  malengo hadi mafanikio.

1. Malengo ni lazima yaandikwe.

Malengo lazima uyaandike sehemu ambayo inaonekana, hapa ni maana ya kwamba uandike sehemu ambayo inaonekana, kufanya hivi kutakuwa kuna kutakufanya malengo hayo uwe unayakumbuka na kujua namna ya kuayatekeleza.

Unaweza ukayaandika malengo hayo kuyaweka katika simu yako katika (screen saver), kioo ambacho unakitumia kujitazama asubuhi na sehemu nyingine ambayo utayaona malengo hayo.

2. Weka vipaumbele katika malengo yako.

Inawezekana fika ukawa na malengo mengi, yaandike malengo hayo katika makundi matatu.

Kundi la kwanza jua yapi ni malengo ya muhimu yapi si malengo ya muhimu, yapi ni malengo ya haraka na yapi sio malengo, na tatu andika malengo ambayo sio ya muhimu sana.

Endapo utagawa malengo hayo utajua ni kipi kinatakiwa kuanza na kipi kinatakiwa kufuata na kwa muda gani.

3. Anza kwa kuanza na hatua ndogo.

Siku zote kama ilivyo ukuaji Wa kiumbe chochote chenye uhai huanza ukuaji wake katika hali ya chini. Kama ilivyo kwa kiumbe yeyote katika ukuaji hata katika ukuaji wa mafanikio yako huanza katika ngazi za chini.

Kitu cha msingi ni kuweza kupanua wigo mpana kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi kwa kila jambo ambalo unalifanya. Na kwa kuwa mafanikio hayana ukomo hakikisha ya kwamba kila iitwayo leo unapata kiu ya kutaka kufanikiwa zaidi.

4. Malengo ni lazima yawe chanya.

Mara kadha watu huwa na ndoto nzuri sana, na pia wengi wao hupanga mambo mazuri kwa ajili ya utekelezaji wa ndoto hizo, ila changamoto kubwa ambayo huwa inakuja ni pale ambapo linakuja suala la utekelezaji wa jambo hilo.

Hapo sasa ndipo utakapoanza kumsikia mtu anasema aaah hivi nitaweza kweli, inatakiwa uondokane na kukata tamaa, vinginevyo kufanikiwa utaendelea kusikia kwa akina  Donald Trump.

5.Malengo lazima yawe katika muda maalumu.

Ni lazima uweke muda kamili kwa ajili ya kutekeleza malengo yako, ifike mahali Malengo yako yafananishe na makampuni yanayohusika ujenzi kwani wao kabla ya kuanza kwa mradi huwa wanafanya mahesabu ili kujua mradi huo wa ujenzi utachukua muda gani mpaka ukamilike.

Ukiishi katika utaratibu Wa kuweka mbinu hiyo itakuwa ni rahisi kwako kutekeleza mambo ambayo unataka kutekeza. Kwa mfano lengo lako ni kujenga nyumba unaweza ukaandika katika lengo lako ya kwamba baada ya muda fulani inabidi uwe umekamilisha ujenzi huo.

Kupanga malengo bila kujua muda Wa kutekeleza malengo ni sawa na bure. Hivyo ni vyema ukajua ya kwamba muda ni mali katika kufanikisha malengo yako kwa wakati sahihi.

6. Malengo ni lazima yawe na mbinu za utekelezaji.

Watu wengi wana malengo ya kusema kwa mdomo tu. Lakini nikwambie ya kwamba ukitaka kufa maskini basi endelea na utaratibu huo Wa kuweka malengo mdomoni.

Kama kweli unataka kufanikiwa hakikisha ya kwamba malengo ambayo umejipangia umeyaandika na kuandika mbinu au njia kwa ajili ya utekelezaji wa malengo hayo.

Kufanya hivi kutakusaidia kujua jinsi ambavyo utayatekeleza malengo hayo ili  kupata mafanikio. Kwa mfano kama malengo yako ni kujenga nyumba basi huna budi kuandika mbinu ambazo zitakusaidia kutengeza nyumba hiyo, pia hapa huenda sambamba na bajeti ya utekelezaji wa malengo yako.

7. Malengo ni lazima yapimike.

Kila malengo ambayo umejipangia Ni lazima yaweze kupimika. Kama nilivyoeleza hapo awali ya kwamba malengo ni lazima yawe na muda maalum kwa ajili ya utekelezaji.

Hivyo ni lazima upime malengo yako ni wapi ambapo umefikia?  Katika muda ambao umepanga kuyatekeza malengo hayo je unahisi utafikia malengo hayo?

Pia uchunguzi yakinifu juu ya malengo yako ni lazima ufanyike ili kujua  fursa na changamoto ambazo zimejitokeza katika kutekeleza malengo yako.

Mpaka kufikia hapa sina la ziada, tukutane siku nyingine.

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako.

PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798-whatsapp

USIOGOPE KUSHINDWA

Habari rafiki;
Katika video yetu ya leo ningependa tuongelee mada inayoitwa USIOGOPE KUSHINDWA.
watu wengi sana wanashindwa kufikia ndoto zao kwa sababu tu wanafikiri watashindwa na watachekwa kwa kushindwa kwao.

Ndugu yangu, katika kusaka mafanikio kushindwa njiani ni jambo la kawaida sana, endelea kupambana hata kama unaona kuna dalili ya kushindwa wewe endelea tu.

Michael Jordan alishawahi kusema;
" I am successful beacause I failed so many times"

Sikiliza video hii fupi upate kujifunza.




Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798

Thursday, January 11, 2018

Jinsi ya kutumia uwoga uliokuwa nao ili kufikia mafanikio makubwa


Woga ni kitu ambacho watu wote wanacho, hakuna mtu anayeishi duniani na ikawa hakuna kitu asichokiogopa na kama yupo mtu wa aina hiyo basi atakuwa ana matatizo ya akili. Lakini kwa wenye akili, kila binadamu duniani lazima atakuwa ana kitu kinachomfanya awe na woga fulani. 

Wengi wetu huwa tunafikiria kuwa woga ni kitu kibaya, lakini ukweli ni kwamba woga si kitu kibaya, kwa kweli woga ni kitu kizuri na ni ishara ya  kuwa unatakiwa kuchukua tahadhari au kujiandaa na hilo jambo linalokutia uwoga. 
Kwa mfano kama huna kazi na umeishiwa na pesa na unatakiwa ulipie pesa ya chumba unachoishi uwoga unakuja. Hivyo unatakiwa ujiandae kwa kwenda nje kupambana na kutengeneza pesa ambayo itakuwezesha kulipa kodi ya chumba unachoishi. Huo ndio uwoga.
Lakini cha ajabu na tofauti ya watu wanaofanikiwa na watu wanaohangaika katika kupata mafanikio ni kwamba watu wenye mafanikio huwa wanajua kwamba kitu ambacho naogopa kufanya ndio natakiwa kukifanya ili kupata mafanikio. Na wale ambao hawafanikiwi huwa wanakimbia ule woga wao, yaani hawapo tayari kufanya kile wanachokiogopa. Kwa kiingereza uwoga unajulikana kama FEAR, herufi hizi zina maana ya kwamba false evidence appear real, ikiwa na maana vitu vya uongo au ushahidi wa uongo unaoonekana kama kweli.
Kwa hivyo ukiogopa kitu huwa unatengeneza picha ambayo si ya kweli. Kwa mfano kama unaogopa kuanza biashara unaweza kutengeneza picha ya kwamba nikifanya hivi watu watanicheka, au pesa yangu itazama au nitashindwa kuiendesha, vitu ambavyo havina ukweli wowote ndani yake. Watu wa saikolojia wanasema “Woga unawaumiza sana watu kuliko kufeli” yaani ni bora ukafanya kitu unachohofia kisha ukafeli kuliko kuwa hujafanya kabisa kwa sababu ya uwoga wako. Hii ni kwa sababu ukifanya kitu hata kama ukafeli lakini tayari kuna mambo utakuwa umejifunza na wakati ujao unaweza kuyakwepa yale yaliyokufelisha mara ya kwanza. Hivyo kama una jambo ambalo sasa hivi unatakiwa ulifanye lakini haulifanyi kwa sababu unaogopa.
Nakuhakikishia kama utafanya maamuzi na kuanza kulifanya hilo jambo  linaweza kukutoa katika matatizo uliyokuwa nayo sasa hivi.
 Watu wengi huwa wanapenda kuniuliza, Pius nifanye nini ili nipate mafanikio, au ni nini siri ya mafanikio?.
HAKUNA SIRI YA MAFANIKIO, Mafanikio ni kufanya tu yale mambo ambayo unatakiwa kufanya lakini unatafuta kila sababu ya kutofanya.
Mfano mzuri hivi karibuni nilitoa challenge kupitia Group la WhatsApp, kwamba kila mtu arekodi video moja inayoelezea biashara yake. Challenge hii niliitoa kwa watu zaidi ya mia tatu (300) lakini, ni mtu mmoja tu ndiye aliyenitumia video aliyorekodi. Baada ya hapo watu wanakuja tena na kuuliza Pius nifanye nini ili nipate mafanikio, jibu ni kwamba fanya kile unachoogopa kufanya utafanikiwa. Kama sasa hivi kuna kitu unaogopa kukifanya anza nacho hicho kila siku.
Nakupa challenge kwamba kila siku ukiamka andika vitu ambavyo unatakiwa uvifanye, kisha angalia ni kipi unakiogopa kati ya hivyo na uanze na hicho. Nakuhakikishia hicho kimoja unachokiogopa ukikifanya kitakupa mafanikio makubwa kuliko vingine. 
Ni mimi ninayejali mafanikio yako;
Pius Justus Muliriye
0754745798
JIUNGE NAMI UPOKEE MAKALA KILA IWEKWAPO MTANDAONI