KILE UNACHOKIPENDA.
Ili
kuwa mtaalamu Fulani, tambua kile unachopendelea. Kitu hicho kimo katika
kuhudumia wengine, hakiko katika kuhudumiwa wewe mwenyewe. Hakiko katika yale
unayoyachukia. Kwa mfano, wengine hawatakuwa wauguzi endapo wanakuza hisia za
kinyaa kusafisha vidonda. Wengine hawawezi kuwa waalimu endapo hawakuzi
uvumilivu na utiaji moyo katika kushughulika na wanafunzi.
Mama lishe anaweza
kukuza ujuzi wake endapo anafurahia kuona walaji wanashiba na kufurahia chakula
chake, na namna anavyo wahudumia.
Kipaji
au talanta ya mama lishe ingekuwa haraka kama walaji wa chakula chake wangekuwa
wazi. Hula na kuondoka kimyakimya. Hawako wazi. Endapo wangelikuwa wanashukuru
na kuelezea kile kinachowaridhisha na kile kinachowakera katika ujuzi wake wa
kuandaa chakula; angelikiboresha zaidi.
Pale
mtu anapopongezwa, napopongezwa, anapotiwa moyo na siyo kusifiwa; akili yake
huhamasika kuboresha utendaji wake.
Ingawa
wapongezaji na watia moyo wanazidi kupungua kutokana na kuongezeka kwa
ubinafsi. Jipime mwenyewe ikiwa ungeliridhishwa na ubora wa huduma au bidhaa
yako. Wahimize wateja waeleze kile wanachodhani kingeboreshwa zaidi.
Kile
kizuri unachopenda, wapo watu wanakipenda pia. Ukifanikiwa kukitoa kwa wingi,
utafanikiwa katika maisha. Ukifanikiwa kukiboresha, utakuwa mtaalamu. Wataalamu wengi wana maisha mazuri; kwa kwa
wanahudumia watu wengi vizuri. Maisha mazuri hutokana na kuhudumia watu wengi
vizuri. Ili uhudumie watu wengi vizuri, kuwa mtaalamu mahiri.
Uaweza KILIKE page yangu FACEBOOK ya THINK BIG START SMALL
Asante kwa kuwa nami;
Nakutakia mafanikio mema na utekelezaji
mwema;
Wasiliana nasi;
Pius J.
Muliriye
0754745798/0657128567

No comments:
Write comments