HII NDIO
MIFANO YA UBUNIFU KATIKA KUJIINGIZIA KIPATO
‘’Maelezo yakikosa picha, ni rahisi kuyasahau. Si lazima picha iwe katika umbo Fulani, hata maandishi yanaweza kubeba picha halisi ya kitu yunachojifunza’’
Ubunifu unalenga kuleta suluhisho la matatizo
ya pande mbili muhimu. Upande wa kwanza ni ule wa kwako na upande wa pili ni
watumiaji wa kile unachobuni. Unapokuwa na nia ya kuishi kwa kujipatia mahitaji
yako vizuri; siri ya kutatua shida zako inabaki moyoni.
Baada ya hapo wafikirie wengine uondoe baadhi
ya shida zao. Tutaona mifano ya ubunifu unaoweza kuondoa shida za wengine. Matatizo ya wengine yanatoa ajira kwako.
Bosi wa biashara yako ni Yule anayeiona
biashara yako kama mkombozi wa shida zake. Vitu vinavoondoa kero au matatizo
kwa watu ni vingi mno na kwa kuwa matatizo nayo ni mengi pia. Usipoweza kutoa huduma au bidhaa kwa watu
wengine unadhani ni nani atakayekuwa tayari kukupatia fedha zake ukazitumie
kuondoa matatizo yako?
Hii ni mifano ya watu waliotumia ubunifu
kutengeneza kipato;
JOHN; MKAZI
WA DAR ES SALAAM
Alipokuwa na umri wa miaka 7, John
alijitambua kuwa hana baba wala mama. John alitambua wazazi wake si hao
aliokuwa naishi nao. Kumbe wazazi wake walifariki kwa ugonjwa wa ukimwi angali
mtoto mdogo. Alikuwa akinyanyasika kwa wazazi wa kambo. Akaamua kutoroka
nyumbani, awe mtoto wa jamii au mtoto wa mitaani.
Alipochoka kuombaomba huko mtaani, akagundua
kuwa, endapo atakuwa na kopo lenye maji, sabuni ya unga, kipande cha godoro na
‘wiper’ anaweza kusafisha vioo vya mbele vya magari, yanapokuwa kwenye foleni
yakisubiri kuruhusiwa na taa za usalama barabarani.
Basi, alianza kusafisha vioo vya magari
madogo kama matatu hivi na kujipatia sh. 200/- kwa kila gari yaani sh. 600/-
kwa kila zamu ya kusimamishwa kwa magari katika barabara aliyopo. Alipata Tsh.
210000/- hadi Tsh. 240,000/-
Ebu jiulize, huu ubunifu si umeleta tija kwa
John? Kiasi hicho cha pesa kinaweza kikawa sawa au kikazidi mshahara wa baadhi
ya wafanya kazi wa umma.
Hii ndio nguvu ya ubunifu. Ebu jiulize, ni
kitu gani unaweza kukifanya na kutatua tatizo la watu na utengeneze pesa zaidi?
kama ulipitwa na video hii, basi nimekuwekea hapa, iangalie unaweza kujifunza kitu;
Asante kwa kuwa nami;
Nakutakia mafanikio mema na utekelezaji
mwema;
Wasiliana nasi;
Pius J.
Muliriye
0754745798/0657128567
No comments:
Write comments