Habari rafiki yangu na msomaji wangu wa mtandao huu wa SHULE TANZANIA;
kabla ya kuendelea na somo au makala ya leo anza kwa kuangalia video hii naamini hutabaki kama ulivyo, utapata somo muhimu sana litakalobadilisha maisha yako kabisa.
KARIBU UTAZAME!
HATUA YA 1.
NAMNA YA KUWA MBUNIFU
Ubunifu ni
uwezo wa kuvumbua bidhaa au huduma mpya ama mbinu mpya za namna ya kukamilisha
jambo kama inavyotakiwa. Uwezo huu upo kwa kila mtu. Namna ya kuujua na
kuutumia ndiyo inayotofautiana kati ya mtu na mtu.
Pamoja na
kuwa sifa ya mjasiriamali halisi, ubunifu ni ujuzi unaoweza kujifunzwa,
kujaribishwa na kutumiwa; hata kama hukuzaliwa nao.
Maisha ya
karne hii ni tofauti na ya karne iliyopita. Katika karne hii ubunifu wa kila
mtu anahitajika sana; hata kama yeye si mjasiriamali au mfanyabiashara.
Ubunifu
unatakiwa kwa wafanyakazi wa kawaida pia. Mfanyakazi hodari ni Yule anayetumia
ubunifu katika kukamilisha majukumu ya kazi zake; kwa haraka na kwa ufanisi.
Ubunifu
wa meneja au mkurugenzi, unahitajika sana katika kubuni na kusimamia
utekelezaji wa mipango ya biashara yake.
Mjasiriamali
naye , hawezi kusonga mbele; kama hakuzi
ujuzi wa ubunifu wake. Ujuzi katika ubunifu ni uwezo wa kutumia maarifa na
mbinu zinzo mhamasisha mtu atambue kile anachoacha kufanya au kinachomshinda
akifanye au akishindwa. Na kwa kukifanya au kukishinda; ubunifu wake utaonekana.
Ubunifu unawawezesha
watu kung’amua fursa zilizojificha na kujiandaa kuzichangamkia haraka.
Hatua za
kujiandaa ni pamoja na kujitayarisha kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia
utekelezaji wa ubunifu mzuri.
Katika sehemu
hii, tutajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ya kuwa mbunifu, hata
kama unadhani hukuzaliwa mbunifu. Sehemu
hii ya kwanza inamaarifa na mbinu za kumhamasisha msomaji atambue uwezo wa ubunifu wake. Ajue namna ya kushinda vikwazo vilivyopo katika ubunifu.
Atumie ubunifu sahihi katika kuanzisha na kuendesha biashara au mradi wowote
kwa mafanikio.
Wako katika Mafanikio
Pius J. Muliriye
0754745798
piusjustus28@gmail.com
No comments:
Write comments