Habari rafiki yangu na msomaji wangu wa mtandao huu wa SHULE TANZANIA;
kabla ya kuendelea na somo au makala ya leo anza kwa kuangalia video hii naamini hutabaki kama ulivyo, utapata somo muhimu sana litakalobadilisha maisha yako kabisa.
KARIBU UTAZAME!
Sio siri kuwa mtandao ni HAZINA kubwa sana ya kupata wateja.
Na hazina hii inazidi kuzalisha wateja siku hadi siku kwa kasi kubwa.
Mfano mzuri ni mtandao wa Facebook wenye watumiajia zaidi ya BILIONI MOJA kwa mwezi na wenye kuingiza mapato ya zaidi ya $ 34,150,000 kwa siku (takwimu za mapato ya Facebook 2014). Mapato hayo yanatokana na matangazo yanayowekwa na wafanyabiashara kama wewe kwenye mtandao wao.
Hii inaonyesha wazi kwamba
mtandao unakupa fursa kubwa sana ya kupata wateja wenye hamu ya kununua bidhaa
na huduma unazozitoa kwakubofya vitufe
viwili vitatu.
Ila cha kushangaza ni kuwa
wafanyabiashara wengi, hususan wakiTanzania japokuwa wanawaona wateja hao
(wenye kuhitaji bidhaa au huduma wanazozitoa) mbele za macho yao, wanahangaika
mno kuwapata. Na sababu kubwa ni zifuatazo:
1. Wanatangazia
Bidhaa Zao Badala Ya Utatuzi Wa Matatizo Ya Wateja Wao:
Kuna mtaalamu
mmoja maarufu wa Mauzo katika Mtandao (online marketer) aitwae Perry Marshal ana msemo wake unaosema,
"Every person who bought a drill NEVER wanted to
buy a drill. They wanted to make holes. If you want to sell drills do not
advertise information about drills, Advertise information about making holes."
Yaani;
"Watu wote waliyonunua drili (ya kutobolea ukuta) hawakutaka
kununua drili. Walitaka kutoboa ukuta. Ukitaka kuuza drili, usitangaze drili,
Tangaza namna ya kutoboa ukuta."
Kwa ufupi, unatakiwa
kuwa mtaalamu mwenye kuwaonyesha wateja wako watarajiwa jinsi ya kutatua
matatizo yao na sio muuzaji mwenye kung'ang'ania kuuza bidhaa zake.
Bidhaa hazitatui matatizo ya wateja wako. Ushauri na muongozo wako kwao ndio yenye kufanya hivyo.
2. Hawajengi Mahusiano Mazuri Na Wateja Wao Watarajiwa:
Japo kuwa mtandao una wanunuzi na wauzaji wengi, umejaa matapeli vile vile. Na mtu asiyekufahamu siku zote atakuona kuwa wewe ni miongoni mwa hao matapeli hususan ukiwa unang'ang'ania sana kuuza bidhaa zako. Ukifanya hivyo wataogopa kukupa pesa zao japokuwa wanahitajia sana bidhaa au huduma unazozitoa.
Ili kujenga uaminifu kwa watu hao, ni vyema kujenga mahusiano mazuri nao kabla ya kujaribu kuwauzia chochote. Ongea nao, wajulie hali, elewa matatizo yao (yanayohusiana na taaluma yako) na kuwa tayari kuwasaidia kwa ushauri na muongozo. Maelezo zaidi ya kufanya hivyo katika nukta ya 4 na ya 5.
Ili kuhakikisha husahau umuhimu wa nukta hii, kumbuka msemo ufuatao:
"Kutangazia bidhaa yako kwa mtu asiyekufahamu ni sawa na kutangazia ndoa kwa mwanamke mzuri njiani asiyekufahamu. Japokuwa unaweza kumfaa katika maisha yake, haitomfanya yeye aache kukupiga kofi"
3. Hawana Taaluma Ya Mambo Ya Mosoko (Marketing)
Haitoshi kuwa na bidhaa au huduma nzuri. Bidhaa au huduma zako hazitojiuza wenyewe. Uwezo wako wa kufanya masoko ndio utaleta mauzo.
Achana na wahenga waliosema 'chema chajiuza, kibaya chajitembeza' na ufuate msemo wa Peter Drucker, mtaalamu na mshauri wa mambo ya uongozi (Management Consultant) aliposema:
"Every business has two primary functions. Marketing & Innovation"
Yaani;
"Kila biashara ina kazi kuu mbili. Masoko na uvumbuzi"
Na kweli. Kazi mbili pekee zenye kuingiza pesa kwenye biashara yako ni Masoko na uvumbuzi. Mambo mengineo yanatoa pesa nje ya biashara yako.
4. Hawana Blogu
Blogu si kwa ajili ya
waandishi wa habari tu wenye mapenzi ya kuandika.
Hapana!
Utafiti unaonesha kuwa
81% ya wafanyabiashara waliokuwa katika mtandao wanaamini kuwa makala za
blogu zao inaleta tija sana katika kuongeza mapato ya biashara yao
[Chanzo: Hubspot]. Na sababu kubwa
ni zifuatazo:
1.
Ina wasomaji wengi kuliko tovuti ya kawaida: Kwa vile blogu inakuwa na majumuisho ya
makala yenye kuelimisha wateja wako watarajiwa, watavutiwa sana kusoma na
kusambaza kwa wenzao wafaidike vile vile.
2.
Inajenga mahusiano ya karibu na wasomaji: Kwa vile makala za blogu zinaonesha
jinsi ya kutatua matatizo ya wasomaji wao, usikilivu na uaminifu
kwao unaongezeka, kitu chenye kurahisisha kuuza bidhaa na huduma
wanazozitoa.
3.
Ni rahisi kukusanya taarifa za mawasiliano (contact information)
za wasomaji kwa ajili ya mawasiliano ya baadae.
4. Wenye ku blogu vizuri huonekana wataalamu
na kuthaminiwa mbele ya macho ya wateja wao watarajiwa kuliko washindani wao.
Kama kweli
upo SERIOUS kupata wateja wengi
kupitia mtandao basi huna budi isipokuwa kumiliki blogu yenye makala mazuri
yenye kuelimisha wateja wako watarajiwa. La sivyo utaachwa nyuma na kupata
wateja kupitia mtandao itakuwa ni ndoto ya mchana.
6. Hawajengi Listi
Ya Wateja Watarajiwa (Lead Generation)
Wataalamu wa masoko ya
mtandao (online marketers) wana msemo maarufu kuhusiana na hili. Wanasema;
"Leads to your
business is like blood to your body.
The less you have, the riskier it is"
Yaani
"Wateja watarajiwa
kwenye biashara yako ni kama damu kwenye mwili wako.
Kila ikiwa pungufu, hatari ndio
inazidi."
Kama hupati watu kila
siku wenye hamu ya kutaka maelezo ya ziada kuhusu bidhaa na huduma
unazozitoa kwenye biashara yako, biashara yako itakuja kufa baada muda mfupi.
Na ndio maana kujenga
listi ya watu hao kwa kukusanya taarifa zao za mawasiliano (contact
information) kama jina, barua pepe na namba ya simu ni muhimu ili upate
kuwasiliana nao mara kwa mara, jambo ambalo linatuleta katika nukta ya 7.
7. Hawawasiliani Na
Wateja Wao Mara Kwa Mara
Kama tulivyoona katika
nukta ya 6, kuwa kutokuwa na listi ya taarifa za mawasiliano ya wateja wako
watarajiwa ni kosa kubwa.
Lakini kosa kubwa
zaidi ni kuwa na listi hiyo lakini huna mawasiliano nao.
KITU KIBAYA SANA
Kama unataka watu hao
wawe wananunua kwako mara kwa mara basi huna budi kuwasiliana nao mara kwa
mara angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki.
Katika mawasiliano
yako wajulie hali, waelimishe na uwape ofa makhsusi kwa ajili yao. Ukifanya
hivyo watakupenda na kukuthamini na watakuwa hawaoni uzito kununua kutoka
kwako.
Nafikiri kwa sasa
ushapata picha halisia kwanini wafanyabiashara wengi wa kiTanzania na wengineo
wanahangaika sana kupata wateja wa bidhaa zao kwenye mtandao.
Usiwe kama wao.
No comments:
Write comments