0657128567

Mwanza Tanzania,

Karibu Sana Kwenye Mtandao huu Wa Shule Tanzania

Tuesday, November 13, 2018

ELIMU YA UJASIRIAMALI BURE

Thursday, September 13, 2018

JINSI YA KUPATA FAIDA HADI MILLION 1 NDANI YA SIKU 30 KUPITIA MTANDAO WA INTERNET!


Habari Rafiki, unaendeleaje??
Nina imani unaendelea vizuri sana, na bado upo katika harakati za kuboresha maisha yako, nipende kukutia moyo tu, kuwa uko katika hatua nzuri ya kufikia mafanikio yako, kwani ili kufikia mafanikio ni lazima kufanya kazi kwa bidii na akili pia.

Katika makala yetu ya siku ya leo ninapenda kugusia ni jinsi gani utafaidika na MTANDAO WA INTERNET na kupata mafanikio makubwa sana ndani ya muda mfupi kwa kazi ambayo unaweza kufanya saa 1 au masaa 2.

Kama umekuwa ukifatilia makala zangu na kazi zangu mbalimbali kupitia kurasa zangu mbalimbali za kijamii kama YOUTUBE, BLOG na FACEBOOK umeweza kuona kazi nazofanya, kazi yangu ni ndogo sana, ni kurekodi VIDEO au kuandika POST kwenye blog yangu kwa muda wa saa 1 au saa 2 kisha napost kwenye mitandao yangu, ndani ya wiki moja zinakuwa zimewafikia maelfu ya watu na hatimaye ninatengeneza kipato kikubwa kupitia kazi zangu hizo.

Unaweza kujiuliza ninapataje pesa hasa ninapofanya yote hayo?? 

Kuna njia nyingi za kufanya ili uweze kupata pesa kupitia mtandao wa internet, lakini sitaweza kueleza zote hapa kwani ni somo pana ambalo unatakiwa kupata muda na kupitia mafunzo hayo. Kama utahitaji kujifunza njia hizo, basi Bonyeza HAPA kupata kozi hiyo online BURE KABISA kupitia darasa langu ONLINE linaloendelea sasa hivi!

Kitu cha msingi siku ya leo ninataka kukupa ushauri ili kama utapenda kufanya kama ninavyofanya mimi basi uweze kutumia mbinu hizi kuingiza kiasi hicho cha pesa au hata zaidi, hii itategemeana na speed yako ya kufanya maamuzi.

Kitu cha kwanza kabla ya kuanza biashara hii ni lazima ujiulize unataka kutatua TATIZO GANI katika JAMII?? hapa wengi ndo hushindwa, wengi wanafikiria kupata pesa mtandaoni ni swala la kubonyeza BUTTON na pesa zinamwagika, ndio maana wengi wameibiwa na kupotezewa muda kwenye biashara za mtandao zinazokuja kila kukicha na kujikuta hawajaambulia chochote zaidi ya kupoteza muda wao.
Ili ufanikiwe kwenye biashara hii ni lazima ujikite katika kutatua matatizo ya watu. Mwandishi mmoja aliwahi kusema,

''Money is a reward after solving somebody's problem''

biashara za namna hiyo ni kama vile fikiria kuhusu Jinsi ya kuwasaidia watu kutatua tatizo la ajira (fundisha watu ujasiriamali kama navyofanya mimi), au kama wewe ni mwalimu tengeneza blog na channel ya youtube anza kuelimisha na kuanza kuuza pamphlets zako na pastpapers, n.k.

Hizo ni baadhi tu ya biashara unazoweza kufanya na ukaanza kuona matunda ndani ya mwezi mmoja au wiki kadhaa.

kitu cha pili ni kujifunza jinsi ya kutumia mifumo ya MTANDAONI ambayo itakusaidia kukusanya watembeleaji kwenye kurasa zako na kukusaidia kukusanya wateja wako watarajiwa kwenye list yako maalumu na hatimaye uanze kutengeneza kipato chako. Usiwaze sana utajifunza wapi yote hayo, mimi nitakusaidia kwa sababu tayari nimefuzu na ndo natumia system hizo mpaka leo ninaendelea kuingiza kipato. ili kupata kozi hiyo BURE bonyeza HAPA utaanza kupata mfululizo wa videos ambazo zitakuwa zinakusaidia kukupa elimu na kukuelekeza njia gani ufate.

Napenda kukupa takwimu za mapato yangu mpaka sasa kupitia kazi nayoifanya mtandaoni;

kupitia Channel yangu ya youtube nimefanikwa kutengeneza Groups 4 za whatsapp ambazo group zote zimejaa watu, nina list ya watu 918 ambao wamelipia sh. 10,000/- kila mtu ili kupata kozi niliyokuwa nikitangaza. hapa ndo utajua Nguvu ya mtandao iko vipi. kwa kozi moja tu nimetengeneza zaidi ya Million 9.

Lakini pia nimefanikiwa kuandika kitabu changu ambacho kinapatikana kwenye mitandao mikubwa ndani na nje ya nchi. Ndani ya Nchi kinapatikana kwenye mtandao wa SIMGAZETI.COM na BECAPI.COM nje ya nchi kinapatikana kwenye mtandao wa AMAZON.COM na sehem zote ninauza SOFTCOPY ya kitabu hicho, na nimefanikiwa kuuza COPY 3200 sawa na Sh. 16,000,000/- 

Kuna baadhi ya watu wanaoniona nikitumia sana mitandao wanadhani napoteza muda lakini kila napojaribu kuwaelezea kuna mafanikio mtandaoni hawaamini kwa sababu wengi wao ni wazembe hawataki kufanya kazi, na ninakwambia wewe unayesoma makala hii kuwa kama  hauko tayari kuamka usiku wa manane na kurekodi video au hata kuandika makala kwa siku za mwanzoni, kazi hii haikufai. Lakini kama wewe ni mchapakazi basi biashara hii inakufaa sana na nakushauri anza kuifanyia kazi mara moja. Uzuri wa kazi hii unafanya kazi kubwa mwanzoni kisha baadae unaanza kula matunda taratibu huku ukiwa umerelax. mimi leo hii bado ninapata pesa kwa video niliyoitengeneza mwaka 2016 mwezi wa 4.

Kama unataka kuanza kazi hii na ungependa nikusaidie kwa kukushika mkono na kuwa karibu na wewe zaidi, na unataka nikupe muda wangu mwingi kukusimamia, basi usisite kuwasiliana na mimi nitakusaidia sana. kuna watu wachache walioamua kuchukua hatua chini ya usimamizi wao tayari wameanza kuona matunda ya kazi hii.

Kama uko tayari Niandikie Ujumbe Whatsapp 0754745798 kisha nitakupangia muda wa kufanya mazungumzo na mimi nikiona unafaa basi nitakusimamia, lakini kama mawazo yako nitaona hayana nia njema basi sitakuwa tayari kukusimamaia, lengo langu nataka vijana tuende na wakati huu wa mabadiliko ya teknolojia, naamini uko tayari sasa.

Tukutane kwenye makala nyingine tena wakati mwingine;
Ni mimi ninayejali mafanikio yako;

PIUS J. MULIRIYE
Whatsapp- 0754745798
www.piusjustus.com

Friday, August 3, 2018


Moja ya mtaji mkubwa ulionao kwenye maisha ni Upekee wako.Tatizo la wengi ni kuwa wanazaliwa hadi wanakufa hawajajua Kitu cha pekee walichonacho.
~~~~~~~
Kwenye kitabu chao cha “Now,Discover Your Strength”(Sasa,Gundua nguvu yako) waandishi Marcus Buckingham na Donald O. Clifton wanasema kila mtu ana uwezo wa kipekee ambao ni zaidi ya watu Elfu kumi wa karibu yake.
~~~~~~~
Unapogundua eneo lako la uwezo wa Kipekee ndio linaitwa “Strength Zone” yako ambayo unatakiwa kuijua na kuwekeza usiku na mchana hapo.Kozi ya kwanza ninayofundisha wanafunzi wangu kwenye MasterMind Coaching Program ya kila mwezi ni kuijua Strength Zone Yako na jinsi ya kuijenga.
~~~~~~~~~
Uwekezaji wenye faida kubwa duniani ni kuwekeza kwenye Strength zone yako.Kadiri unavyowekeza basi ndivyo Kadiri thamani yako inaongengezeka.
~~~~~~~~~~
Je,Umeshaijua Strength zone yako tayari?

Chukua hatua sasa!

Pius J. Muliriye
Whatsapp | 0754745798

Friday, July 27, 2018

DON'T WAIT UNTILL THINGS GET READY!

Nilikutana na huyu mtu James mwang'amba back 2009, alikuwa akifundisha somo la self development kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na nilipata bahati ya kuhudhuria mafundisho yake kwa siku 2 mfululizo!



Alizungumza kitu ambacho kili stick katika kichwa changu ambapo alisema USISUBIRI MPAKA MAMBO YAWE SAWA KUPIGANIA NDOTO ZAKO!!

Kwa mara ya kwanza sikumuelewa kabisa, kwa sababu nilikuwa nikifikiria huwezi kufanikiwa ukiwa katika nchi maskini kama Tanzania, huwezi kufanya lolote bila serikali kukutengenezea mazingira, na nilikuwa miongoni mwa watu wanaolalamika sana nikiona mambo hayaendi sawa!
.
.
Baada ya miaka mitatu wakati napitia makablasha yangu nikakutana na notebook niliyoandika masomo aliyokuwa akifundisha, nikakutana na sentensi hiyo tena iliyokuwa ikisema " Don't wait untill this get ready"...

Hapo ndipo nilipoanza kujitafuta mimi ni nani!

Siku hiyo nilipata wazo la kuandika kitabu ili niweze kushea na watanzania ujuzi nilionao na niliamini kabisa kitabu changu kingewasaidia wengi!

Nilimshirikisha rafiki yangu nikamwambia nataka niandike kitabu hiki ninaamini kitauzika sana na watu watanufaika na mimi nitanufaika pia, alicheka sana akaniambia hivi wewe unawajua watanzania???? Tangu lini watanzania wakawa wasomaji wa vitabu?? Nakuhakikishia hutauza kitabu hata kimoja unapoteza muda na nguvu zako achana na wazo hilo, kwanza gharama za kuzalisha kitabu hicho ziko juu sana hutaweza kabisa.πŸ˜’

Kusema ukweli alinikatisha tamaa, nikaanza kuwaza upya juu ya maoni yake, lakini nikakumbuka kabisa mwalimu wangu James Mwang'amba aliniambia kijana "Usisubiri kabisa mambo yawe sawa ndio uchukue hatua" ndipo nilipojiambia sitasubiri mpaka watanzania wapende kusoma vitabu ndipo niandike.....!! Nikaanza mara moja kuandika na nikakamilisha kitabu changu ndani ya mwezi mmoja!

Shida nyingine ikaja, Sina pesa ya kupublish kitabu changu pamoja na kuzalisha copy nyingi na kusambaza, nikakwama na nikaacha na kuendelea na mambo mengine!!
.
.
Lakini mwaka 2017 mwezi wa kwanza nikapata wazo ambalo lilinifanya nishindwe kulala kabisa, nikakumbuka kuwa nina simu ya smartphone, nima laptop ambayo nilinunua wakati nipo chuo kikuu lakini vikawa havinisaidii chochote, ndipo nilipoanza kuvitumia na kuanza kusoma wenzetu nchi za nje wanafanya nini!..

Nikapata mwanga na nikaanza sasa kufanyia kazi elimu ile niliyoipata na mwaka huo huo mwezi wa nne nikafanikiwa kufungua channel yangu ya Youtube na nikarekodi video yangu ya kwanza kwa kutumia simu yangu ya mkononi nikizungumzia kitabu changu na faida zake na kukitangaza kwa atakayehitaji kupata ujuzi huo nitamtumia kwenye whatsapp au email yake.....Sikuamini macho yanguπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Nilipata oda nyingi sana, na sasa video ile ina views zaidi ya 20,000 na nimeshauza copy takribani 3650 mpaka sasa bila gharama ya kutoa copy wala usambazaji, copy zote nimetuma nikiwa ndani kwangu, kwenye gari nikiwa nasafiri, nikiwa kijiweni napiga story na marafiki zagu n.k. hii ndio nguvu ya TEKNLOJIA, wewe unatumiaje mapinduzi haya ya teknolojia??

Siku hizi watu hawahangaiki kufanya malipo MPESA, TIGOPESA n.k ziko kila mahali mtu akipenda kitu hasumbuki kulipia, tumia nafasi hiyo utafanikiwa.

Nakushauri wewe kijana mwenzangu, mazingira yasikifanye ushindwe kupigania ndoto yako, usisubiri serikali itengeneze mazingira ya biashara ndipo ufanye, wakati huo fursa itakuwa si yako tena, isome jamii yako ina matatizo gani kisha tafuta jawabu la matatizo yao na maisha yako yatabadilika.

Asanteni sana na niwatakie siku njema!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Pius J. Muliriye
www.piusjustus.com

Monday, June 11, 2018

MAFUNZO BURE [JINSI YA KUTUMIA MTANDAO WA INTERNET KUANZISHA AU KUKUZA BIASHARA YAKO]

Hellow Rafiki, natumai unaendelea vizuri na harakati za kukomboa maisha yako, naamini kabisa unafanya juhudi za makusudi kufikia lengo hilo, na nikupongeze sana sana!

Kama ambavyo nimekuahidi kuwa nimekuandalia kozi maalumu ambayo itakusaidia wewe kama kijana ambaye una malengo makubwa sana katika maisha yako.

Kozi hii ni moja ya kozi muhimu sana ambayo itakusaidia kupiga hatua kubwa katika maisha yako na kwa haraka zaidi kuliko njia nyingine yoyote ile ambayo umeshawahi kuitumia.

Katika kozi hii nitakuonyesha siri kubwa sana ambayo mimi nimeitumia kuingiza kipato kikubwa zaidi kupitia mtandao wa internet, njia hii inatumika sana na wenzetu wa nchi za magharibi ambao tayari wana uelewa mkubwa sana katika mtandao wa internet, njia hii inatumika katika nchi za Marekani, na ulaya na hata nchi nyingine ambazo zimepiga hatua katika elimu hii ya mtandao.

Hii ni njia mabayo ni rahisi sana kuitumia kama mtu  ana nia ya kutaka kupiga hatua katika maisha yake.
Ebu fikiria, tangu siku imeanza hadi unapoenda kulala umeangalia TV kwa muda gani kulinganisha na simu yako ya smartphone????
Naamini kabisa umetumia muda mwingi  sana kwenye simu yako, na unatumia simu yako kufanya mambo mengi ikiwemo kupata Habari na Burudani pia.

Katika kozi hii nitakufundisha jinsi unavyoweza kutumia simu yako ya mkononi (Smartphone yako) au komputa yako kuingiza pesa huku ukiwa umelala.

Naomba nitoe ONYO katika hili; sikufundishi njia ya mkato kutengeneza pesa, njia hii nayokufundisha inahusisha kufanya kazi na si kulala tu, utaweza kulala na kurelax ukiwa umeshatengeneza mifumo yako vizuri mtandaoni na itakuwa ikifanya kazi badala yako huku wewe ukiendelea kufanya mambo mengine.

Kama uko tayari kuanza mafunzo haya, basi naomba nikupe vigezo. Ili uweze kupata kozi hiyo vizuri ni lazima simu yako iwe na vitu vifuatavyo!

  • Application ya MESSENGER (facebook messenger)- Hii ni ile application ya kusomea ujumbe kupitia facebook. Application hii ni muhimu sana kwani utakuwa ukipata series za video za mafunzo hayo kupitia messenger hiyo. Kama hauna application hiyo  nenda mara moja PLAYSTORE kwenye simu yako kisha DOWNLOAD applicationa hiyo na uanze mafunzo mara moja.
  • BANDO la kutosha. Hakikisha simu yako ina bando la kutosha kuweza kuangalia video hizo nitakazokuwa nakutumia kila siku.
  • CHAJI ya kutosha.
Hayo ni baadhi ya mahitaji ambayo simu yako lazima iwe nayo  ili kupata kozi hii.

Ndani ya kozi hiyo utakuta link ya kujiunga na GROUP yetu ya WHATSAPP ambako utaendelea kupata mafunzo zaidi na kama una maswali utajibiwa kikamilifu huko.

Sasa unaweza kuingia darasani rasmi. Kujiunga tafadhari bonyeza picha hii chini utaanza kupokea ujumbe kutoka kwetu moja kwa moja!



Asante sana, nitafurahi kukuona darasani!
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

Pius J. Muliriye
0754745798
www.piusjustus.com

Monday, May 21, 2018

SAIKOLOJIA YA WATU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Habari rafiki, natumai unaendelea vizuri na harakati za kukomboa maisha yako na kuelekea katika uhuru wa kifedha.



Katika mfululizo wa mada zetu juu ya jinsi ya kutumia mtandao wa internet kibiashara leo hii ninakuletea mada inayozungumzia Saikolojia ya watu walioko katika mitandao ya kijamii.

Kama tunavyojua, katika mitandao ya kijamii ni sehemu ambako watu hukutana na kujumuika pamoja, kuchati, kuonyesha style mbalimbali za maisha, kwa kulitambua hilo ninapenda kukwambia rasmi kuwa katika mitandao ya kijamii SIO MAHALI PA KUUZIA BIDHAA YAKO AU SIO MAHALI PA KUFANYIA BIASHARA YAKO.

Hii ni sawa na kuwakuta watu wako katika club wanacheza mziki na kuponda raha halafu wewe unaingia na bidhaa zako na kuanza kuwatangazia ili wanunue, nakuhakikishia watakufukuza na hata kukupiga kwa sababu unawaharibia starehe zao.

Kwa hiyo, kama wewe umekuwa ukiweka picha za bidhaa zako kila mahala kwenye mitandao ya kijamii acha mara moja tabia hiyo.

KAMA NDIO HIVYO, NINI UFANYE??

Badala ya kupost picha za bidhaa na kuwatangazia watu wanunue, tengeneza JUKWAA LAKO/KIJIWE CHAKO na huko ndiko utumie kuwaelimisha juu ya umuhimu wa bidhaa unayoitoa na kisha uwauzie, itakuwa rahisi kununua kwa sababu wameshapata elimu juu ya hiyo bidhaa kutoka kwako. Hivyo ndivo unapaswa kufanya.

JUKWAA NI NINI??
Jukwaa katika biashara ya mtandao ni sehemu maalumu ambako unatumia kuwaelimisha watu kuhusu jambo flani. Jukwaa linaweza kuwa;


  • Facebook messenger chat Bot (messenger)
  • Facebook group
  • Whatsapp group
  • Email list 
  • Youtube subscriber etc
Tumia platform hizo kukusanya watu na kisha waelimishe kisha toa ofa yako.

JINSI YA KUJENGA JUKWAA LAKO

Jukwaa linajengwa kwa kutumia software ambazo zinaruhusu watu kuweza kuingia automatically na kisha ujumbe unakuwa unawafata mara kwa mara kulingana na ulivyoset wewe.

Kama utahitaji kujua zaidi na jinsi ya kuweza kujenga na kutengeneza jukwaa lako kitaalamu nimekuandalia kozi maalumu iliyopo kwenye mfumo wa video zikielezea kwa kina hatua kwa hatua jinsi ya kuset program hizo.

Kama utakuwa tayari kujifunza zaidi ili uanze kutengeneza kipato kupitia mtandao basi jaza fomu hii chini tukishapokea fomu yako tutawasiliana na wewe moja kwa moja na tutakupa utaratibu wa kuanza kozi hiyo.





Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;

PIUS J. MULIRIYE
0717375782 | WHATSAPP
0754745798 | CALL | TEXT

Sunday, May 13, 2018

MAMBO MATATU (3) YA KUFAHAMU KABLA YA KUWA MJASIRIAMALI WA MTANDAO.

Habari rafiki, nafurahi kuwa pamoja na wewe siku ya leo tena ambapo ninakwenda kushea  na wewe mambo ya msingi sana unayotakiwa kuwa nayo kabla ya kuwa mjasiriamali wa mtandao.

Kabla ya yote jana nilirusha video iliyokuwa inaonyesha jinsi nilivotumia mtamdao wa internet kutengeneza hadi million 7 na zaidi kupitia mtandao wa internet, kama hujaiona nitakuwekea mwisho wa makala hii uweze kuitazama.

Tuendelee na mada yetu ya siku ta leo, mada inasema mambo matattu ya msingi ya kufahamu au ya kuwa nayo kabla hujaanza kuwa mjasiriamai wa mtandao.

Mjasiriamali wa mtandao maana yake ni kwamba, mtu au kampuni inatoa huduma au bidhaa kupitia mtandao wa internet.

Mambo hayo ni:-

1. WAZO (TATIZO LA KUTATUA.)
Hii ni moja ya kitu muhimu sana mtu yeyote anayetaka kuingiza pesa kupitia mtandao anatakiwa awe nayo. Ni lazima uwe umeabaini tatizo linaloisumbua jamii na una njia ya kuweza kulitatua, kama huna huwezi kutengeneza hata senti moja mtandaoni, nitakushauri uendelee kuchati tu kama wanavyofanya wengine.

2. MPANGO
Baada ya kuwa na wazo au umebaini jamii iliyoko mtamdaoni ina tatizo gani weka mpango thabiti wa jinsi ya kutatua tatizo hilo. Hili ndio jambo muhimu kabisa kwani hapa unaandaa mikakati ya kuweza kusaidia tatizo hilo kabla hujajitokeza mtandaoni na kutangaza.

Mpango unaweza kukusanya taarifa sahihi za jinsi ya kutatua tatizo hilo (HOW TO...) baada ya hapo unaweza kwenda kifua mbele na kujibrand sasa mtandaoni na pesa zitakufuata tu.

3. JUKWAA (PLATFORM)
Hapa ndio kuna pesa, kama huwezi kujenga jukwaa basi hata kama una wazo zuri, au umeandaa mpango mzuri bado hutaweza kuingiza chochote, kwani jukwaa ndio kitu cha msingi sana.

Jukwaa hujengwa kwa utaratibu maalumu ambao unatakiwa ujifunze ni jinsi gani utaweza kujenga jukwaa ambalo litaweza kukulipa maelfu ya pesa.

Jukwaa linaweza kuwa FACEBOOK MESSENGER BOT, YUTUBE CHANNEL AU WHATSAPP GROUP, majukwaa hayo kuna utaratibu wa kuweza kuyajenga na yakakuletea tija. Hili ni somo refu sana na unatakiwa ujifunze kwa kina.

Baada ya kuwa na vitu hivyo muhimu sasa unaweza kuingia mtandaoni na utatengeneza pesa nyingi sana.

Tambua kuwa huduma za mtandao Tanzania inakuwa kwa kasi kubwa sana, watu wengi wapo kwenye mitandao ya kijamii na kila mtu ana matatizo yake na wanahitaji kujua jinsi ya kuyatatua, nani wa kuweza kuyatatua??? Jibu sahihi ni wewe na si mtu mwingine.

Baada ya kusema hivyo mimi kama mmoja wa watu wachache wanotumia mtandao vizuri kibiashara nimeanzisha darasa la kufundisha vijana wenzangu wanaopenda kutumia mtandao kwa tija kujiingizia kipato na kwa njia halali kabisa, darasa hilo litakuwa kwenye group ya whatsapp, kama unataka kujifunza basi unakaribishwa, bonyeza picha hii chini kuingia darasani, wahi sasa nafasi ni chache.
Pia kama nilivyokuahidi kukuwekea ile video, kama hujaisikiliza unaweza kufanya hivo hapa chini.



Asante kwa muda wako, tukutane darasani.
Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako;


Pius J. Muliriye
0717375782|whatsapp only
piusjustus28@gmail.com


JIUNGE NAMI UPOKEE MAKALA KILA IWEKWAPO MTANDAONI